Saturday, January 9, 2021

MARAFIKI KUTOKA NEW YORK WAFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KUTOA POLE WASHINGTON DC


NY Ebra kutoka NEW YORK akiwa Washington DC kutoa pole nyumbani kwa familia ya Editha. Editha Lyimo ni dada yetu alietutoka ghafla sikuya tar 26. 

Hapa ni watoto wa marehemu mtoto wake wa kwanza wa kike, Hope  na wa kiume Henry pamoja na  mama wa marehemu, Ny Ebra aliambatana na marafiki wengine kutoka New York, Adella Mwakasekele, Goston, Vick na Fatma.
 

*IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU YA EDITHA LYIMO*

Tujumuike na wanafamilia katika Ibada ya Misa ya kumbukumbu na kuaga mwili wa mpendwa wetu siku ya Jumamosi January 23, 2021 saa 8 mchana (2Pm) itakayofanyika katika anuani

The church Address is below.

Berean Baptist Church

924 Madison St, NW

Washington, DC 20011

Misa itaendeshwa na Bonaventura Mwaipaja msaidizi wa mchungaji Mbatta kutoka kanisa la Kilutheri lugha ya Kiswahili, Rockville.

Wakati wa ibada tumeruhusiwa wahudhuriaji 50 na lazima uwe umevaa barakoa (mask)

Wakati wa kutoa heshema za mwisho hakuna idadi. Watu wataruhusiwa kuingia na kutoka. Wahudumu mlangoni wata simamia kuhakikisha hakuna zaidi ya watu hamsini.

Kufika kwako ndio kufanikisha safari ya mwisho ya Editha Lyimo.

Ukipata taarifa hii tafadhali mtaarifu na mwenzio.

*BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA NA JINA LAKE LIHIMIDIWE*

No comments: