Friday, January 8, 2021

TWITTER WAIFUNGA RASMI AKAUNTI YA RAIS TRUMP


Mtandao wa Twitter umemfungia moja kwa moja Rais Donald Trump kuendelea kutumia mtandao huo kwa sababu anautumia kinyume kuhatarisha usalama wa raia.

Twitter umeripoti leo Ijumaa kwamba wamefuatilia kwa karibu maandiko ya Rais Trump na kugundua maandiko yake yanaviashiria  kuchochea vurugu.

Siku ya Jumatano Twitter na facebook walimfungia Rais Trump akaunti zake kuzuia madhara ya wafuasi wake waliovamia jengo la Bunge na kusababisha watu 5 kupoteza maisha akiwemo afisa polisi wa Bunge hilo lakini baadae walizifungua akaunti zake siku inayofuata.

Na hiki ndicho kilichosababisha Twitter kufunga akaunti yake

" The 75,000,000 Great American Patriots who voted for me, AMERICA FIRST, and MAKE AMERICA GREAT AGAIN , will have  a GIANT VOICE  long into the treated unfairly in any way, shape or form!!!"

Na muda mfupi baada ya hapo akaandika "To all of those who have asked, I will not be going to Inauguration on January 20th"

Baada ya maandiko hayo Twitter walilazimika kufunga akaunti ya Rais Trump moja kwa moja 

No comments: