Advertisements

Monday, March 8, 2021

Mawaziri Afya Waikubali Immuno Booster Kupambana na Changamoto za Upumuaji

Wakati Watanzania wengi wakipambana na maradhi mbalimbali yanayosababisha changamoto za upumuaji, ikiwemo nimonia na Corona, mawaziri wawili wa afya, wameipigia chapuo dawa ya Immuno Booster inayozalishwa na JKBRS na kufurahishwa na uwezo wake wa kupambana na magonjwa ya changamoto za upumiaji na kupandisha kinga ya mwili.

Kwa nyakati tofauti, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Doroth Gwajima na naibu wake, Dk. Godwin Mollel walikutana na Mkurugenzi wa JKBRS, Tabibu Riziki jijini Dodoma na kupata wasaa wa kumsikiliza akiwafafanulia kuhusu dawa hiyo iliyotengenezwa kwa mitishamba.

Kwa upande wake, Waziri Gwajima alimpongeza Tabibu Riziki kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kuelekeza nguvu zaidi katika dawa za mitishamba zenye uwezo mkubwa wa kutibu maradhi mbalimbali, ikiwemo changamoto za upumuaji na kuwahamasisha Watanzania watumie dawa hiyo sambamba na kufuata maelekezo mengine ya wataalamu wa afya katika kujilinda na maradhi mbalimbali, ikiwemo kulinda kinga za miili yao.
Naibu Waziri Gwajima naye alimpongeza Tabibu Riziki na kuwahamasisha Watanzania kuitumia dawa hiyo, sambamba na kuwataka wengine wanaoshughulika na ugunduzi wa dawa za mitishamba, kuendelea kuumiza vichwa kutafuta dawa zitakazomaliza kabisa changamoto za upumuaji na magonjwa mengine kama Corona kwa Watanzania.

Kwa upande wake, Tabibu Riziki alionesha kufurahishwa na jinsi viongozi hao wa juu kartika wizara ya afya walivyoipokea dawa hiyo na kuongeza kuwa Watanzania wanapaswa kuichangamkia kwani ni tiba sahihi katika wakati sahihi kama huu ambao taifa linapambana na magonjwa ya changamoto za upumuaji pamoja na maradhi mengine.

“Dawa hii ya Immuno Booster inatengenezwa kwa virutubisho asilia vyenye uwezo wa kuongeza madini ya Calcium na Vitamini C. Pia virutubisho hivi husaidia kukinga na kuulinda mwili dhidi ya saratani, maambukizi ya virusi ikiwemo Flu, SARS, Covid 19 na kujikinga na uvimbe na miwasho mbalimbali mwilini.

“Kama hiyo haitoshi, Immuno Booster inasaidia kuongeza kinga kwa watu wenye aleji mbalimbali za mafua, ngozi na kubanwa na kifua na hata watu wenye changamoto za upumuaji Immuno Booster huwasaidia sana,” anaeleza Tabibu Riziki.

“Ofisi zetu zipo Ubungo Plaza, ‘ground floor’ kwa jijini Dar es Salaam lakini dawa zetu zinapatikana nchi nzima kupitia kwa mawakala wetu. Unaweza kuwasiliana nami kwa namba za simu 0744111115 au 0753185 592,” anahitimisha Tabibu Riziki

GPL

No comments: