Advertisements

Friday, April 9, 2021

CAG ABAINI UPIGAJI MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA (TPA)

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu ripoti za mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2020.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu ripoti za mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2020 akiwa pamoja na wajumbe wa wa Kamati ya Hesabu za Serikali
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya LAAC,Mhe.Grace Tendega ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati wa ripoti za CAG mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2020,Kushoto kwake ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere na kulia kwake ni Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali Mhe.Deus Sangu
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Japhet Hasunga ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu ripoti za mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2020.

Na.Alex Sonna,Dodoma

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amefanya ukaguzi maalum katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kubaini kuwepo kwa mapungufu kadhaa ikiwemo upotevu wa mapato kwa kutoa msamaha usiostahili wa Dola za Marekani 979,126.5 kwa Kampuni ya Saruji ya Mbeya.

Hayo yamebainishwa leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya CAG kwa wandishi wa habari jijini Dodoma ambapo ambaini pia kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu wa malipo ya Sh Bilioni 3.76.

Akizungumzia ukaguzi huo wa TPA, CAG Charles Kichere amesema April 30, 2018 menejimenti ya TPA ilipeleka kwenye Bodi ya Usimamizi maombi ya msamaha wa Dola za Marekani Milioni 1.52 kuiombe kampuni ya saruji Mbeya kwa ajili ya wateja wake waliopo Burundi na DR Congo wanaosafirisha saruji kupitia Bandari ya Kasanga.

Amesema Kampuni hiyo ilieleza kuwa wateja wao walipata changamoto ya kukosa meli za kuja Bandari ya Kasanga kuchukua shehena za saruji zao walizokua wameagiza na hivyo kupelekea shehena hiyo kuharibika.

Amesema April 17, 2019 kupitia azimio la Bodi ilitoa msamaha wa asilimia 100 kama ilivyoombwa hivyo kampuni hiyo ya Saruji Mbeya ilipaswa kulipa Dola za Marekani 50,000 kama gharama za utunzaji wa shehena hizo na Dola za Marekani 7,726 kwa ada tu ya kuondolea shehena.

Bw. Kichere amesema ukaguzi wake uliangalia ukweli wa msamaha uliotolewa na uligundua shehena ya tani 1,445 (mifuko 28,904) ambayo iliharibika katika Bandari ya Kasanga ilikua na malimbikizo ya gharama ya Dola za Marekani 543,224 iliyostahili kutolewa msamaha.

” Maombi ya msamaha yaliyopelekwa katika Bodi April 14, 2019 yalikua ya Dola za Marekani Milioni 1.52 yakijumuisha madeni ya saruji iliyoharibika ya Dola za Marekani 543,244 na gharama za utunzaji Dola za Marekani 979,126 kwa shehena zilizosafirishwa kutoka Bandari ya Kasanga katika kipindi cha Januari 2013 na Oktoba 2017 na hakukua na hasara iliyopatikana na hivyo kutostahili msamaha.

Kuchukulia shehena nzima ya tani 1445.2 kama imeharibika na kutoa msamaha wa Dola za Marekani Milioni 1.52 badala ya gharama sahihi ya Dola 543,244 kuliisababishia hasara TPA ya upotevu wa mapato wa Dola za Marekani 979, 126.59.

Kwa pande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali Japhet Hasunga alimpongeza CAG kwa ripoti yake huku akisema kama Bunge wataifanyia kazi katika kusimamia mali za Serikali kutokana na ripoti hiyo kuonyesha mapungufu.

“Ripoti hii imeonyesha mapungufu mengi ikiwemo matumizi mabaya ya fedha ,ubadhirifu hivyo kama wabunge wataisimamia na kuishauri serikali ili kuweza kuondoa vitendo hivyo.

No comments: