Advertisements

Tuesday, April 20, 2021

MPINA AMVAA CAG HASARA ATC

*Ahoji kwanini sababu ya hasara ya bilioni 60 ATCL haikutajwa aomba Kamati ya PAC kumbana zaidi ili ukweli ujulikane*
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE
wa Kisesa, Luhaga Mpina ametilia shaka ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa namna ilivyoripoti hasara ya sh. bilioni
60 kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kusababisha mkanganyiko
mkubwa kwa wananchi.

Mpina
amesema kwa mujibu wa Taarifa ya CAG inaonesha kuwa Kampuni ya ATCL
ilipata hasara ya sh. bilioni 60 mwaka (2019/20), sh. bilioni 23
(2018/19) na kwamba sababu ya hasara hiyo iliyotajwa na CAG ni matumizi
yanayohusisha usafirishaji wa abiria na mizigo kuongezeka kwa asilimia
45 kutoka sh. bilioni 133.6 mwaka 2018/2019 hadi kufikia sh. bilioni
193.6 mwaka 2019/2020.

Pia
ripoti hiyo ilieleza mapato yaliongezeka kwa asilimia 41 kutoka sh.
bilioni 116 hadi sh. bilioni 157.6 lakini cha kushangaza sababu za
kuongezeka kwa matumizi hayo hazikuwekwa kwenye ripoti ya CAG licha ya
kuwa zinafahamika wazi na kusababisha mkanganyiko mkubwa kwa wananchi.

Mpina
amesema sababu hizo ni pamoja na kutokea mlipuko wa Covid-19 katika
kipindi cha mwaka 2019/2020 na kuathiri usafiri wa anga ambapo hapa
nchini ndege zilikuwa zinafanya kazi kwa asilimia 20 tu.

Kampuni
ya Air Tanzania iko kwenye mageuzi makubwa ambapo katika mwaka
2019/2020 ndege mpya 2 aina ya Boeing na Bomberdear zilinunuliwa na
ndege zingine zilinunuliwa mwishoni mwa mwaka wa fedha 2018/2019 na
hivyo kupelekea gharama za uendeshaji na utunzaji kuongezeka.

Pia
ndege zinazotumiwa na Shirika la Air Tanzania zimekodiwa kwa Wakala wa
Ndege za Serikali na hivyo Kampuni inalazimika kulipa gharama ya
ukodishaji kwa wakala huyo.

Kutokana
na kuongezeka kwa ndege Shirika limelazimika kuajiri marubani na
watumishi wengine ili kukidhi mahitaji ya utoaji huduma .

Katika
kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 Shirika liliongeza kituo kipya cha
nchini cha Mpanda na kufungua kituo nje ya nchi cha Mumbai India, Pia
shirika liliongeza miruko katika vituo vya Dodoma, Mwanza na
Kilimanjaro.

Pia Kampuni
ya ATCL ina deni la miaka ya nyuma la sh. bilioni 217 ambapo inalazimika
kulipa riba kila mwaka na mwaka huu wa 2019/20 shirika limelipa riba
ya deni sh. bilioni 12.5 ikilinganishwa na malipo ya riba ya sh. bilioni
8 ya mwaka 2018/2019.
Kampuni ya ATCL imeanza mageuzi ya uwekezaji miaka miwili tu iliyopita na hivyo sio rahisi kupata faida leo.

Pia
amewatoa wasiwasi wananchi kuwa Kampuni yetu ya ATCL inazidi kuimarika
na kuwataka wanaobeza kwa namna moja au nyingine waache na badala yake
wapende vitu na mafanikio ya nchi yao.

Mpina
amebainisha ushahidi wa kampuni yetu kuimarika na mafanikio
yaliyopatikana kwani kabla ya hatua hizi kuchukuliwa na Serikali ya
awamu ya tano shirika lilikuwa halina uwezo wa kulipa watumishi wake
mishahara hivyo Serikali ililazimika kulipa mishahara yote kwa 100%
lakini tunapozungumza leo Shirika letu linajitegemea kulipa mishahara ya
watumishi wake kwa 87%.

Katika kipindi cha ukaguzi shirika lilikuwa na ukwasi wa bilioni 17.5 huu ni ushahidi kuwa kampuni yetu inaendelea vizuri
Kampuni
imeajiri marubani waliofikia 80 na wote ni wazawa wakiwemo marubani
wanawake ambao wote tunawaona wakirusha ndege zetu kwa umahiri mkubwa.

Pia
kwa kufanya ulinganifu na makampuni mengine ya kigeni mfano Kenya
Airways (KQ) ambapo Kampuni ya KQ toka mwaka 1977 inaendelea kupata
hasara kila mwaka lakini Serikali yake inaendelea kuwapa fedha za
kuendesha shirika hilo kwa kutambua kuwa faida za usafiri wa anga ni
mtambuka.

Kuongezaka kwa
idadi ya watalii nchini ni ushahidi mwingine wa mafanikio ya shirika
letu ambapo watalii wameongezeka kutoka milioni 1.1 (2015) hadi milioni
1.5 (2019) na mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka Dola za
Marekani bilioni 1.9 (2015) hadi Dola za Marekani bilioni 2.6 (2019).

Huduma
za biashara na uwekezaji nchini zimekuwa na ufanisi mkubwa najua
watanzania hawajasahau abiria, bidhaa na mizigo yote kutoka nchini kwetu
ilitegemea ndege za nje mfano. Mbogamboga, Maua, Samaki, Mabondo, Nyama
kwenda masoko ya nje najua hatujasahau na hatutasahau.

Faida
nyingine ni kuwahisha wagonjwa kupata matibabu ndani na nje ya nchi kwa
gharama ndogo baada ya kununua ndege zetu mfano zamani mgonjwa
alitakiwa kupelekwa India lazima apitie kwanza Dubai kuunganisha ndege
za India kwa gharama kubwa na kutumia muda mrefu lakini baada ya kununua
ndege zetu na kuanzisha ruti ya India gharama ya usafiri imepungua kwa
asilimia 40 na muda umepungua kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwahi kwenye
huduma.

Kuhusu usimamizi
na uendeshaji wa Shirika la ndege Tanzania ni Mpina ameshauri
watanzania wenzetu wanaobeza Kampuni yetu ya ATCL waache mara moja.

Pia
Serikali ilipe deni la nyuma la ATCL la sh bilioni 217, Serikali
iendelee kuwekeza kwa kuongeza idadi ya ndege za abiria na mizigo,
kupanua na kujenga viwanja vipya vya ndege, kuongeza safari, marubani na
kukarabati miundombinu muhimu mingine muhimu hii ni pamoja na ujenzi
wa uwanja mpya wa ndege Mkoa wa Simiyu.

No comments: