Advertisements

Wednesday, April 14, 2021

WAZIRI BASHUNGWA ATETA NA MKURUGENZI WA MAWASILIANO KAMPUNI YA TANZANIA DAIMA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) amekutana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Tanzania Daima Gerva Lyenda (Kushoto) Leo April 13, 2021 Dodoma. Mkurugenzi huyo alifika ofisi za Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na Michezo na kupata nafasi ya kufanya mazungumzo na Mhe. Bashungwa kuwasilisha ombi lao na kwa majadiliano zaidi kuiomba serikali kama itawezakuwapa leseni ya kuanza kazi ya kuchapisha tena gazeti la Tanzania Daima ambalo lilizuiliwa leseni yao tangu June 24, 2020.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari alifuta leseni ya gazeti hilo ikiwa ni baada ya kulionya gazeti mara kadhaa huku gazeti lenyewe lililazimika kuomba radhi. Kufuatiwa kufungiwa huko Mkurugenzi Lyenda alimueleza Waziri Bashungwa kuwa “gazeti limeajiri watu 90 na wanahangaika kwakukosa leseni tumejifunza na hatutorudia makosa” na akaongeza kwakushukuru “Asante kwa kutusikiliza hii ni fursa kubwa kwetu, maana miezi zaidi ya nane ni mingi sana na hatujafanya kazi yoyote.

Waziri Bashungwa amewapa wito wakuheshimu tasnia ya habari kwakuwa wote tunajenga nchi moja na kuongeza kwa kusema “watanzania wa sasa wameamka wanajua lipi ni baya na lipi ni zuri sasa kama unatoa habari zakupotosha tu utakuwa unawakosea haki yao ya kuhabarishwa”. Pia Waziri ametoa wito kwa wadau wa tasnia ya habari kuunga mkono dhamira ya Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassani kuona haki ya uhuru wa habari inaendana na wajibu na uzingatiaji sheria, kanuni na misingi ya taaluma ya habari.

No comments: