Advertisements

Tuesday, May 4, 2021

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEJUMUIKA NA WANANCHI WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KATIKA FUTARI ALIYOWAANDALIA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi ya Msahafu uliotolewa na Masheikh wa Mkoa wa Kaskazini Unguja akikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari maalum ilioandaliwa kwa Wananchi wa Mkoa huo.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika Futari Maalum iliandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkokotoni Unguja.(Picha na Ikulu )
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na kutowa salamu za Mkoa wakati wa hafla ya Futari Maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa Wananchi wa Mkoa huo.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh.Salum Gharib baada ya kumalizika kwa Sala ya Magharibi iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja mkokotoni, wakati wa hafla ya futari ilioandaliwa na Rais kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Haroun Ali Suleiman na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume.(Picha na Ikulu)

No comments: