Advertisements

Tuesday, August 3, 2021

MHE. RAIS SAMIA ASHIRIKI CHAKULA CHA JIONI NCHINI RWANDA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi na Wananchi wa Rwanda, kwenye Hafla ya Chakula cha Jioni kilichoandaliwa kwa ajili yake na Rais Kagame Mjini Kigali Rwanda leo Agosti 02,2021. Mhe. Rais Samia yupo Nchini Rwanda kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitambu cha kumbukumbu alipotembelea Makumbusho ya Hifadhi ya Kimbari Kigali Nchini Rwanda leo Agosti 02,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, wakati wa Chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Rais Kagame Mjini Kigali Rwanda kwa ajili yake leo Agosti 02,2021. Mhe. Rais Samia yupo Nchini Rwanda kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili. IKULU.

No comments: