Advertisements

Thursday, September 16, 2021

James Rugemalira Aachiwa Huru

Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP na aliyekuwa mmiliki mwenza wa IPTL, James Rugemalira aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kuifuta kesi hiyo.

Mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yakimkabili Rugemalira, yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai.

Rugemalira na mwenzake, Harbinder Sethi walikuwa wakikabiliwa na mashitaka 12 yakiwemo ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya jumla ya takriban shilingi bilioni 358 ambapo walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 19, 2017 ambapo makosa hayo walidaiwa waliyatenda Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic Tawi la Kati Kinondoni.

Aidha, awali kulikuwa na mazungumzo na ofisi ya DPP ili kukubaliana namna ya kulipa fidia ili waachiwe lakini baadaye mazungumzo hayo yalivunjika.

Juni 16, 2021, Seth aliachiwa huru kwa masharti ya kutotakiwa kutenda kosa lolote kwa kipindi cha mwaka mmoja huku pia akitakiwa kulipa fidia ya sh. bilioni 26.9 kwa serikali ya kuingia makubaliano na DPP ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kwa njia muafaka.

GPL

No comments: