Advertisements

Monday, October 25, 2021

MTAMA WAINGIZIA WAKULIMA SH.BILIONI 9

Mkuu wa Ofisi Ndogo ya Shirika la Mpango Chakula Duniani (WFP), Neema Mina Sitta akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Program ya Kilimo Himilivu cha Mtama (CSA), ilivyotengeneza mamilionea kwenye wilaya za Bahi, Kongwa na Mpwapwa mkoani Dodoma.
Ofisa Ufuatiliaji Msaifizi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), William Laswai akimuonesha Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi, Janeth Joseph Mtama bora uliozashwa na wakulima wa mkoa wa Dodoma kupitia Program ya Kilimo Himilivu cha zao hill.

Na Mwandoshi Wetu, Dodoma

WAKULIMA 22,000 wa zao la Mtama, kutoka Wilaya za Kongwa, Bahi na Mpwapwa, wameuza tani 17,000 za zao hilo kwa msimu wa mwaka huu na kufanikiwa kujipatia Sh bilioni 9.

Wakulima hao wamenufaika na kilimo hicho kupitia Program ya Kilimo Himilivu cha Mtama (CSA), inayotekelezwa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kupitia Mpango Mkakati wa 2017 hadi 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Ofisi Ndogo ya WFP, Neema Mina Sitta alisema kwa sasa wamefikia vijiji 203 kati ya zaidi ya 700 vilivyopo.

Alisema WFP ni mpango ambao unafanya kazi kwa mtazamo wa kibinadamu kama kusaidia sekta ya kilimo, maendeleo, wakimbizi, afya na lishe ambapo kwa Dodoma wameweza kusaidia wakulima wa zao la Mtama kuongeza usalishaji.

Sitta alisema WFP iliandika mradi wa kilimo himilivu katika wilaya za mkoa wa Dodoma na kupata ufadhili wa Sh. bilioni 1.7 kutoka Shirika la Maendeleo la Ireland (Irish Aid) ambapo matunda yameshaonekana kwa wakulima zaidi 22,000 kujpatia Sh bilioni 9.

Alisema uamuzi wa WFP kuingia katika kilimo himilivu cha Mtama wameweza kuunganisha wakulima na soko moja kwa moja na kuondoa madalali au watu wac katikati walikuwa wanachangia kushusha bei ya zao.

Mkuu huyo alisema kwa sasa bei ya zao la Mtama kilo moja inaunzwa hadi Sh 550 kutoka Sh 250 ya awali hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na kuhamsisha kilimo hicho.

Alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima namna ya kulima kilimo bora na endelevu ambacho kitaweza kuingiza mapato yao na nchi.

Sitta alisema kilimo cha Mtama ambacho kinalimwa katika mkoa wa Dodoma kinazingatia mfumo wa kilimo hai jambo ambalo linachangia kuwepo na uhakika wa soko kote duniani.

Mkuu huyo wa ofisi ndogo alisema ushiriki wao kwenye kilimo ni kuhakikisha mkulima ananufaika na kilimo lakini pia ardhi inakuwa endelevu kwa vizazi vijavyo.

“WFP kupitia ufadhili wa Irish Aid, tumefanikiwa kuongeza uzalishaji wa zao la Mtama ambapo kwa msimu huu wakulima wamezalisha zaidi ya tani 17,000 na kujipatia Sh bilioni 9 lakini hitaji ni kubwa zaidi hasa kutoka ndani na nchini Sudani Kusini,” alisema.

Alisema kwa msimu ujao wanatarajia uzalishaji kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa wilaya za Chemba, Kondoa, Dodoma na Chamwino.

Sitta alisema katika kutekeleza CSA wamekuwa wakishirikiana na Serikali kwa kutumia watalam wao wa kilimo hali ambayo inaleta ufanisi mzuri.

Halikadhalika alisema wamepokea ombi la Serikali katika kuanzisha program zakuongeza uzalishaji kwenye zao la alizeti ambapo matarajio yao ni kuingiza kwenye Mpango Mkakati wa WFP wa 2022 hadi 2027.

Aidha, alisema WFP imekuwa ikinunua mazao mengine kama mahindi kwa ajili ya kupeleka katika ofisi za WFP za nchi nyingine na kwenye kambi za wakimbizi za Nduta na Nyarugusu.

Sitta alisema hadi sasa wamefanikiwa kununua zaidi ya tani laki saba kwa ajili ya kusambaza katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

No comments: