Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022. Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman
Kinana akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo katika Kikao cha
pamoja na Wajumbe wa CHADEMA, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana mara baada ya Kikao kilichofanyika Ikulu
Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja
na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe,
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel
Chongolo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na Baadhi ya
Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Baadhi ya Viongozi wa CCM pamoja na
Serikali Ikulu Chamwino tarehe 20 Mei, 2022.
No comments:
Post a Comment