Advertisements

Thursday, July 7, 2022

NBAA YAENDELEA KUTOA ELIMU MAONESHO YA BIASHARA YA SABASABA


Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA Leonard Mkude akisikikiza maelezo kutoka kwa Afisa  wa NBAA Humphrey Symphorian kwenye Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)  katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA Leonard Mkude akisaini kitabu kwenye Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)  katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam
Afisa kutoka Bodi ya NBAA, Humphrey Symphorian(kushoto)  akitoa maelezo kwa Twity Robert aliyefika kwenye Banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ili kupata elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam
Afisa kutoka Bodi ya NBAA, Deodatus Soka(wa pili kulia) akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam. Wa kwanza kulia ni Afisa kutoka Bodi ya NBAA, Humphrey Symphorian.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Temboni wanafunzi wa kidato tatu na nne wakisikiliza elimu iliyokuwa inatokewa na maofisa wa Bodi ya NBAA katika  Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam
Afisa kutoka  Bodi ya NBAA, Michael Mwakifuna(wa kwanza kulia0  akitoa maelezo kuhusu mitihani ya Bodi inavyofanyika wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam
Maonesho yakiendelea
Maafisa kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)  wakiwa kwenye picha pamoja kwenye banda la Bodi hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Bodi hiyo lililo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha Sabasaba ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician) mpaka ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama na makampuni ya kihasibu na Kikaguzi. 

Pia NBAA wanatoa huduma zote ikiwemo jinsi ya kujisajili kufanya Mitihani, malipo ya Ada kwa Wanataaluma, ametoa wito kwa wote wanaotaka kufanya usajili kwenye Bodi ya NBAA kufika katika Banda lao lililopo ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Amesema Bodi hiyo kwa sasa mfumo wa kidijitari wa kutoa huduma zake hususan usajili wa wanafunzi na Wananchama kupitia tovuti yao, amesema huduma hizo zinapatikana hata ukiwa sehemu mbalimbali pia kwa sasa huduma hizo zimehamia Sabasaba.


No comments: