Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Shirika lisilo la
Kiserikali la SHINA INC limeweza kuwafunda vijana kuhusu kujitabua kwenye suala la elimu pamoja
na ukatili na unyanyasaji wa Kijinsia. Kongamano hili limefanyika Makunduchi,
Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika
kujenga Maendeleo endelevu.
Akizungumza wakati wa kufunga Kongamano hilo Rais wa Shirika
la SHINA INC, Jesca Mushala amesema vijana wengi wanapata elimu kwa ajili ya
kwenda kuajiliwa lakini hii ni tafsiri ambayo inakwamisha vijana wengi hapa
nchini.
Amesema Elimu itakutayalisha wewe kwenda kujiajiri au
kutafuta matumizi ya familia maana enzi za nikimaliza nakwenda kupata ajira
hakuna kwaiyo nawategemea wanakongamano kuwa cachu wa maendeleo kwa kuanzisha
ajira ili kuwainua vijana wengine kwa kuwa mshumaa unawasha mshumaa mwingine na
ndio ilivyo katika maendeleo.
“Mtu akimaliza chuo anasubiri kuajiriwa kwasababu amefanya maombi ya kazi na anakaa kabisa kwa kutulia, huko ni kutotumia akili ulizozipata darasani, huko tunakotoka ana shahada mbili au tatu akajifunza vizuri kilimo na sasa yuko shambani analima na anasomesha watoto wake pamoja na kuendesha maisha ni kwasababu alikwenda darasani kusoma ule ujuzi alioupata darasani ndio anauendeleza mtaani” alisema Mushala
Pia alisisitiza vijana wengi wanasema kuwa nitajiajiri vipi
wakati sina mtaji au sijawezeshwa lakini wanasahau kuwa waliwezeshwa na wazazi
kwa kuwapeleka shule kwenda kuongeza ujuzi wao na kuna muda ukiona unaweza
kunyanyuka na wengine basi unaweza kuungana na vijana wenzako ili mkanyayuka
pamoja.
“Elimu sio tu ile unayoipata darasani bali kuna elimu
unayoipata mtaani mfano kama hili kongamano linatoa elimu ya namna kujitambua
na kuna vijana wengi wamefanikiwa kupitia program mbalimbali za SHINA INC na
kwa sasa wamefika mbali ila inabidi vijana kujiepusha na elimu ambayo haiendani
na maadili au utamaduni wa Kitanzania “ alisema Mushala
Pia amesema ili kusaidia kupunguza ukatili wa kijinsia na
unyanyasaji ni mtoto wa kiume na mtoto wa kike wafundishwe kwa pamoja maadili
na utamaduni wa Mtanzania kwa maana kwamba huwezi kumfundisha mtoto wa kike
peke yake kwa kumueleza masuala ya ndoa, elimu pamoja na kujitambu bila
kumfundisha na mtoto wa kiume kwani ili kupunguza unyanyasaji wa Kijinsia.
“Mtoto wa kiume akifundishwa vizuri ataweza kuthamini mtoto
wa kike ili kusudi kesho yake asiweze kumnyanyasa mke wake.” Alisema Mushala
No comments:
Post a Comment