Advertisements

Sunday, July 3, 2022

WAZIRI DKT MABULA AMKABIDHI TUZO RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi tuzo ya heshima Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete mkoani Arusha mwishoni mwa wiki. Tuzo hiyo alikabidhiwa kwa niaba ya Kikwete wakati wa Mkutano wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2022 huko Kisumu nchini Kenya.
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akingalia tuzo ya heshima aliyokabidhiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula mkoani Arusha mwishoni mwa wiki. Tuzo hiyo ilitolewa kwa Kikwete wakati wa Mkutano wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2022 huko Kisumu nchini Kenya.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akisoma maelezo katika cheti alichokabidhiwa na tuzo ya heshima Rais Mstaafu Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki mkoani Arusha. Tuzo hiyo ilitolewa wakati wa Mkutano wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2022 huko Kisumu nchini Kenya.
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akingalia Medali aliyokabidhiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kwa niaba yake. Tuzo hiyo ya heshima ilitolewa wakati wa Mkutano wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2022 huko Kisumu nchini Kenya. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

 Na Munir Shemweta, ARUSHA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amemkabidhi Rais Mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete tuzo aliyokabidhiwa wakati wa Mkutano wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2022 huko Kisumu nchini Kenya.

Tuzo aliyokabidhiwa Kikwete ni tuzo ya heshima iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa) ikiwa ni kutambua juhudi zake za kuimarisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Commitment in Fevour of the African Movement of the Territorial Government)

Dkt Mabula alimkabidhi Tuzo hiyo mkoani Arusha mara baada ya halfa ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mfuko wa Wanyamapori Afrika (AWF) yaliyofanyika Julai 1, 2022 katika Kituo cha Urithi wa Utamaduni.

Waziri wa Ardhi alimueleza Rais Mstaafu Kikwete kuwa, wakati alipohudhuria mkutano wa wa tisa wa viongozi wa Majiji huko Kisumu nchini Kenya alikabidhiwa tuzo hiyo kwa niaba yake kutokana na juhudi alizozionesha wakati wa utawala wake kwenye masuala ya mamlaka ya serikali za mitaa.

Kwa upande wake Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alimshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula kwa kuonesha uaminifu wa kuitunza tuzo hiyo tangu alipokabidhiwa Mei mwaka huu hadi alimpomkabidhi.

Wakati wa mkutano wa majiji maarufu kama Africities uliobeba kauli mbiu ya mchango wa miji inavyoweza kuchangia utekelezwaji wa dira ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na Umoja wa Afrika mwaka 2063 mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo hali ya miundo mbinu kwenye miji na namna bora ya kuimarisha maisha ya wakazi wa miji hiyo.

Mameya wa miji mbalimbali, Mawaziri wa serikali za mitaa walihudhuria mkutano huo kwa lengo la kutafuta suluhu ya changamoto zinazowasumbua wakazi wa miji yao kama vile mipangilio mibaya ya majengo, mitaa pamoja na changamoto za upatikanaji wa umeme.

Majiji mengine iliyowahi kuandaa mkutano wa aina hiyo unaofanyika kila baada ya miaka mitatu tangu1998 jijini Abidjan, ni Johannersburg, Dakar Kule Senegal na Marakesh Nchini Morocco.

No comments: