Advertisements

Monday, May 29, 2023

WANACHUO WA CHUO CHA KIISLAMU CHA MOROGORO WATEMBELEA NBAA

 

Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akiwakaribisha wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro waliotembelea Bodi hiyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
 Afisa Tawala na Rasilimali watu NBAA, Gloria Kaaya akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno wakati wa ufunguzi wa ziara ya  wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro walipotembelea ofisi za Bodi hiyo ili kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi ikiwa ni kujijengea ufahamu wa kutosha juu ya masuala ya Uhasibu na Ukaguzi.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akizungumzia majukumu mbalimbali ya Bodi hiyo kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro walipotembelea ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa NBAA, CPA Mohammed Nusra akitoa ufafanuzi namna wandaaji wa hesabu wa dini ya Kiislamu wanavyotakiwa kuendana na uandaaji wa hesabu za fedha wa Kitaifa na Kimataifa  kwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro waliotembelea ofisi za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa NBAA, Humphrey Symphorian akizungumza kuhusu namna wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wanavyoweza kijisajili na kufanya mitihani ya Bodi pale watakapomaliza au wakiwa chuoni.
Baadhi ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wakiuliza maswali kwa wataalamu kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) mara baada ya kupata mafunzo walipotembelea Bodi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwanachuo wa Mwaka wa Tatu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro anayesoma Uhasibu Shaban Issa Abdallah akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanachuo wenzake mara baada ya kupata mafunzo kutoka kwa wataalam wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
Baadhi ya wanachuo wanaosoma masomo ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wataalamu kutoka  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wakufunzi pamoja na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wanaosoma masomo ya Uhasibu mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyofanyika katika ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

No comments: