Thursday, September 26, 2024

RC SINGIDA ABORESHA TAARIFA ZAKE KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA



Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego akionesha Kadi yake ya Mpiga Kura baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaloanza Uboreshaji Septemba 25,2024 na litadumu kwa siku saba mkoani Singida hadi Oktoba mosi mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa aliboresha taarifa zake katika Kituo cha Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye ulemavu Sabasaba leo Septemba 25,2024.

Akixungumza baada ya kumaliza uboreshaji, Mhe.Dendego aliwahimiza wananchi wa mooa wa Singida kujitokeza kwa wingi kujiandikisha lakini pia kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati huu ambao Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeweka kambi mkoani humo.

Amesema ni muhimu kila mwanasingida mwenye Sifa kujitokeza na kujiandikisha ili apate fursa ya kujiandikisha katika Daftari hilo ili apate fursa ya kuchagua viongozi anaowataka wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (kushoto) akiangalia kadi ya Mpiga Kura aliyokabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego mara baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Wapiga Kura katika uboreshaji ulioanza jana mkoani Singida.Wananchi wa Mkoa wa Singida wameanza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Septemba 25, 2024 hadi Oktoba 1, 2024.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake