Thursday, September 26, 2024

UTENDAJI WA PSPTB WAPENGEZWA NA WAJUMBE WA BARAZA

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo lililofanyika mkoani Morogoro.
Katibu mkuu wa TUGHE mkoa wa Dodoma , Samweli Nyungwa akitoa salamu za uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania ( TUGHE ) wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo.
Mwenyekiti wa TUGHE PSPTB, Shilla Mwandu akizungumza kuhusu namna wafanyakazi wanabidi kujitadhmini pale wanapokuwa wanafanya kazi za Serikali wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB lililofanyika mkoani Morogoro
Mkurugenzi wa mafunzo wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Amani Ngonyani akijibu hoja za wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa PSPTB ili kuboresha Utendaji kazi wa Bodi hiyo kwenye kikao cha Baraza hilo kilichofanyika mkoani Morogoro
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Amos Kazinza akizungumza jambo kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB lililofanyika mkoani Morogoro
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa PSPTB wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa kwenye kikao kazi kilichokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi hiyo pamoja na wageni waalikwa wakati wa wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo


Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imefanya kikao cha Baraza la wafanyakazi leo ili kujadili mafanikio, mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa bajeti mwaka uliopita ya 2023/2024.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu Ununuzi na Ugavi Godfred Mbanyi amesema baraza ni chombo kinachoundwa na sheria ya Mahusiano kazini kwa ajili na kuweka mazingira mazuri mahali pakazi ambapo chombo hiki kinawiwa kwa mkataba baina na Menejimenti pamoja na chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi.

Pia amasema baraza la leo limefanyika ili kutathmini utendaji kazi wa bajeti ya mwaka uliopita ya 2023/2024, kisheria na kiutaratibu bajeti yoyote kabla haijahidhinishwa lazima ipitishwe na Balaza la Wafanyakazi sehemu ya kazi.

Mbanyi amesema Bajeti ya mwaka 2023/2024 ilikamilika toka Juni 30 hivyo ni wajibu wa menejimenti kuja kueleza balaza nini mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa bajeti iliyokamilika muda wake.

“Umuhimu wa Mabaraza ya kazi kwanza yanaleta ushirikishwaji wa wafanyakazi sehemu ya kazi hivyo wafanyakazi wanakuwa ni sehemu ya maamuzi katika taasisi, kwaiyo taasisi sio kwamba inakuwa inaongozwa na Menejimenti lakini inakuwa na chombo ambacho kinawakilisha wafanyakazi wote katika taasisi mbalimbali.” Alisema Mbanyi

No comments: