Advertisements

Monday, August 31, 2015

CHADEMA MOSHI MJINI WATANGAZA ILANI YA UCHAGUZI YA JIMBO LA MOSHI MJINI.

Meneja Kampeni wa mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema na UKAWA,Jafary Michael ,Bw Raymond Mboya akifanya utamburisho mbele ya wanahabari wa mkutano wa mgombea huyo na wanahabari uliofanyika katika Hotel ya Keys.
Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro ambao ni wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini wakiwa katika kikao na mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema na UKAWA,Jafary Michael.

MKWASA ASEMA STARS IPO KAMILI


Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema vijana wake wapo tayari kuwavaa Nigeria Septemba 05, 2015 katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017. 
Mkwasa ambaye yupo nchini Uturuki na kikosi cha timu ya Taifa kambini kwa mazoezi ya takriban wiki moja, amesema vijana wameonyesha mabadiliko makubwa baada ya kupata wiki moja ya mazoezi ya pamoja. 
“Mazoezi wanayofanya hapa yamewajenga stamina, unaweza kuona wanacheza kwa nguvu muda wote, wanakaba na kushambulia kwa pamoja, hii ni dalili nzuri ya vijana kuelekea katika mchezo huo dhidi ya Nigeria”amesema Mkwasa. 
Kocha huyo wa timu ya Taifa amesema timu yake imefanya mazoezi katika nyanja zote ikiwemo mazoezi ya kujenga mwili na kucheza mpira wa kasi. 

MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA NDANI YA WILAYA YA NJOMBE MKOANI NJOMBE.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ludewa mjini kabla ya kuanza kuwahutubia ,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo na kuhudhriwa na maelfu ya watu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Ludewa waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo.

PSPF WATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA LIGI YA MADEREVA WA BODABODA WA KIPUNGUNI JIJINI DAR

 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya G Unity Fc kwa ajili ya mchezo wa fainali uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B katika kata ya Kipunguni manispaa ya Ilala jijini Dar. Ambapo timu ya G Unity FC waliibuka washindi baada ya kuichapa timu ya Sukuma Land Fc bao 5 kwa 2.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya Sukuma Land FC wakati wa mchezo wa fainali wa kombe la Madereva bodaboda wa kata ya Kipunguni.Wa pili kushoto ni ASP Mbunja Matibu kutoka Traffic Makao Makuu.

UN YAFANYA USAFI SOKO LA TEMEKE STEREO KUADHIMISHA MIAKA 70

IMG_5298
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) kabla ya kuanza zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
IMG_5365
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ikiwemo kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa wananchi na wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo mwishoni mwa juma. Kushoto ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini, Patric Otto. Wa tatu kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Temeke, Sophia Mjema, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira manispaa ya Temeke, Ally Hatibu.

Sunday, August 30, 2015

LOWASSA AUNGURUMA MKOANI IRINGA

Sehemu ya Wafuachi wa CHADEMA na Vyama vinge vinavyounda UKAWA wakiupokea msafara wa Mgombe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ulipokuwa ukiwasili Mafinga Mjini, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 30, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, IRINGA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapumbia maelfu ya wananchi wa Mji wa Mafinga, Wilayani Mufindi Mkoani Iringa, waliokuwa wamefurika kwa wingi  kwenye Uwanja wa Wambi, Mafinga Mjini, Mkoani Iringa Agosti 30, 2015.

DURHAM WACHANGIA JIJI LA ARUSHA KWA KUFANYA ONESHO LA SABA SABA FAIR TRADE

Mrs Nturu mmoja ya waandaji wa saba saba fair trade iliyofanyika Jumapili Aug 30, 2015 jijini Durham, North Carolina kwa ajili ya kuchangia mji wa Afrusha ambao ni mji dada na mji wa Durham.
Mmoja ya wajasiliamali akionyesha bidhaa zake kwa wageni waliofika.
 Nashona akimwelekeza mmoja ya wageni waliofika leo jinsi ya uvaaji khanga.

David Mngondo akiongea na  mmoja ya wageni wahudhuriaji saba saba day.

Meza nyingi ya familia ya Kitanzania wakitangaza bidhaa zao.

DK. FAUSTINE NDUGULILE AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI VIJIBWENI‏

Mgombea ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia CCM, Dk. Faustine Ndugulile akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mzima uliopo Kata ya Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam jana.
Wananchi wakifurahia alipokuwa akipanda jukwaani mgombe ubunge kupitia CCM, Dk. Faustine Ndugulile.

UCHAGUZI WA MWAKA HUU TANZANIA HAUNA MDAHALO WA UGOMBEA NAFASI YA RAIS?

Nimekuwa nikifuatilia taarifa mbalimbali kuhusu uchaguzi utakao fanyika tarehe 25 October lakini sijasikia tetesi kama kutakuwa na mdahalo wa ugombea nafasi ya urais. Inawezekana upo lakini mimi sijasikia na kama ni hivyo basi wanaohusika kuuandaa wahabarishe wananchi.

Huu mdahalo unahitajika sana ili tuweze kuwajua vizuri hawa wanaotaka kuwa viongozi wetu. Wagombea wote wa vyama vinavyo shiriki wakutanishwe waulizwe maswali ya msingi (live) tuweze kupima majibu na uwezo wao. Midahalo ni imekuwa inapewa umuhimu mkubwa sana kwa nchi za wenzetu. Yawezekana kuna ambao wana sera nzuri lakini hatujapata nafasi ya kuwasikiliza. Uwezo wa kujieleza kwa kiongozi ni kitu muhimu sana. Pamoja na kwamba ahadi zinazo tolewa majukwaani huwa hazitimizwi zote, na hili siyo Tanzania tu bali hata nchi zilizo endelea; lakini pale mtu anapotamka anakuwa recorded. Mtu anaye kaa kimya ni ngumu kumwelewa na hutaweza kumhoji kwa kile ambacho hakutwambia au kuahidi.

MDAHALO UITISHWE

Rais Kikwete ahudhuria jubilei za watawa Lugoba

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Sista.Perpetua(kushoto) aliyekuwa anaadhimisha miaka 50 ya utawa na Sista Ponsiana(kulia) aliyekuwa anaadhimisha miaka 25 ya utawa .Maadhimisho hayo yalifanyika katika kanisa Katoliki Lugoba jana.(picha na Freddy Maro).

VAZI LA KHANGA LA ASYA IDAROUS DURHAM, NORTH CAROLINA

VIJIMAMBO NA ASYA IDAROUS KHAMSINI IWATOA SHUKURANI SANA KWA MANANC


 Watanzania wa North Carolina wakipata picha ya kumbukumbu kwenye khanga party iliyofanyika siku ya Jumamosi Aug 29, 2015 mji wa Durham, North C
 Mashabiki wa mama wa mitindo wakipata picha ya kumbukumbu na Asya Idarous Khamsini 
 Picha ya kumbukumbu
 Mashabiki wakiselebuka

CHAMA CHA ACT-WAZALENDO CHAZINDUA KAMPENI ZAKE VIWANJA VYA MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM LEO

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es Salaam leo.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia katika uzinduzi huo.

SIMBA YAFUNGWA KWA MBIINDE NA YANGA DMV YAKUBALI YACHAPWA 5-2

Watanzania na marafiki zao wakijumuika kwenye nyama choma kabla ya mechi ya Simba na Yanga iliyochezewa Hyattsville, MD siku ya Jumamosi Aug 29, 2015 na Simba kukubali kipigo cha boa 5-2 na kuendelea kuwa wateja Yanga DMV. Timu hizi uundwa na mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi DMV.
Nyama choma ikiendelea
Timu ya Simba DMV
Timu ya Yanga DMV

Helikopta ya Nyarandu Anogesha Kampeni za Mgombea Mwenza CCM

Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la  Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la
Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Helkopta ya mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini ikitua. Helkopta ya mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini ikitua.Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa kampeni na kuacha kushangaa helkopta. Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa kampeni na kuacha kushangaa helkopta.

HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU

Wagombea wa UKAWA na Mwenyekiti wa UKAWA wakionyesha kitabu chao cha Ilani ya Uchaguzi wa 2015.

Hotuba ya Lowassa

Jangwani, Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015

Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu

Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.

Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.

MAKUNDI 10 YAPENYA NUSU FAINALI DANSI 100%

Wasanii wa Kundi la The W.D kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% 2015 lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oystebay Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana wanaunda kundi la Timu Makorokoro wa wilaya ya Temeke jijijini Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robof wa shininali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana wanaaunda kundi la timu ya Shamba kutoka Temeke wakionyesha umahiri wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay jijini Dar es Salaam ,mwishoni mwa wiki.Shindano hilo iliandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania. Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.

Kichupa cha leo Jux - Looking For You (Official Music Video) ft. Joh Makini

African in New York Episode 23

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UWEKAJI WAZI WA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA KATIKA MIKOA YOTE YA UNGUJA NA PEMBA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba kuanzia tarehe 03/09/2015 hadi tarehe 07/09/2015 ili Umma uweze kupata nafasi ya kulikagua Daftari la Awali na kutoa taarifa za kufanyiwa marekebisho pale inapostahili.

KESI YA TALAKA YA MMILIKI WA ST. MATHEW YAAHIRISHWA TENA

court_gavel
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala, Dar es Salaam, imepanga Septemba Mosi mwaka huu kutoa hukumu katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali zenye thamani ya Sh Milioni 800 inayomkabili Mmiliki wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks, Thadei Mtembei.
Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa juzi lakini iliahirishwa kutokana na upande wa mlalamikaji kutofika mahakamani.
Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Rajab Tamambele alisema kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya hukumu na kwamba itaendelea Septemba Mosi mwaka huu.
Mlalamikaji Magreth Mwangu anaiomba mahakama imuamuru mdaiwa kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa yeye na watoto wake.
Katika kesi hiyo, upande wa mlalamikaji ulikuwa na mashahidi wanne wakiwamo watoto watatu aliozaa na Mtembei ambao wanasoma katika shule za St Mary’s International na Hijra Seminari ya Dodoma.

Saturday, August 29, 2015

MKUTANO WA UKAWA JANGWANI
Ahimidiwe MUNGU aletaye Wokovu. Ashukuriwe MUNGU atupaye yele tumwombao. Atukuzwe MUNGU atazamaye kila Mnyonge na kumfariji.
Posted by UKAWA Seattle Washington STATE on Saturday, August 29, 2015

Lowassa kiboko yao, Jangwani yatapika

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa, Mh Edward Lowassa akiongea na wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani mapema leo.Mh Lowassa amesema kipaumbele chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni za busara na hekima bila kutumia matusi.
Mke wa Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Mama Regina Lowassa akitoa salamu kwa wakazi wa Jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani leo.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Duni Haji akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Ukawa leo katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza katika uzimduzi wa Kampeni za Ukawa zilizofanyika Jangwani leo.