Monday, May 23, 2011

Professor wa Maryland University avutiwa na kipaji cha Azile Charles

Professor wa Maryland University alivutiwa na kipaji cha Azile Charles alipopelekewa Video yake iliyowekwa kwenye Blog yaVijimambo kutoka youtube na Mtanzania ambae hakutaka kutajwa jina lake.Professor ameahidi kumpa Scholarship chuoni hapo lakini alikua anatakakujua kama amemaliza High school na kama ndio ataweza kupatikana wapi.

Azile aligunduliwa na mtandao wa Global Publishers siku alipozungumuza na mtandao huo,Gaucho (jina la mcheza soka mahiri wa Brazil, Ronaldinho Gaúcho) huyo wa ‘Mji Kasoro Bahari’ alidai ana uwezo mkubwa wa kusakata soka lakini amekosa vifaa vya kufanyia mazoezi na kukosa nafasi ya kuonekana kwa wapenda soka.

Blog ya Vijimambo inaomba yeyote mwenye habari zake asisite kuwasiliana na djlukejoe@gmail.com,Asante

1 comment:

  1. ushauri, na hii ni kama bado hujafanya, peleka hii habari global publisher, facebook, u-turn, michuzi, darhotwire....etc ili wakusaidie kumtafuta huyu dada

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake