Monday, October 24, 2011

DC NYALUGUSU KUUMANA NA BONGO REAL JUMAPILI OCTOBER 30,2011

DC Nyalugusu Sports Club
Bongo Real Football Club
Mechi ya DC Nyalugusu na Bongo Real itachezwa October 30,2011 kwenye wanja la Meadowbrook park.
Mpambano huu unaosubiriwa na wachezaji na viongozi wa timu  zote kwa sababu Bongo Real wanataka kuonyesha kufungwa kwao mechi ya mwisho na DC Nyalugusu ilikua bahati mbaya,mpambano huu uliochezewa Meadowbrook Park July 23,2011 DC Nyalugusu waliibanjua kwa taabu Bongo Real 6-1.

Timu Kepteni wa Bongo Real(chama Kubwa) amewataka wachezaji kufika mazoezini Leo Jumatatu,Jumanne,na Jumatano  iku ya Alhamisi inaonyesha itanyesha mvua na hali ya hewa itarudi safi tena siku ya Ijumaa,Jumamosi ni mapumziko na Jumapili mtanange wenyewe.wachezaji wa Bongo Real ushindi uanzia kwenye mazoezi tufike kwa wingi 

Kocha wa DC Nyalugusu(wazee wa dozi),Jabir Jongo amesema kwao mazoezi yanaendelea leo Jumatatu kama kwaida na mechi hii tutawahakikishia mashabiki mnapata burudani tosha kwani sisi ndio wazee wa dozi. kufungwa kwetu na Cameroon sio kigezo cha kufungwa na Bongo Real,sisi kwetu Bongo Real ni kama kumsukuma mlevi.

Mpambano huu unatarajiwa kua mgumu na mkali.

1 comment:

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake