Wadau picha hizi zinatisha lakini mtuwie radhi kwani ndiyo hali halisi iliyotokea usiku wa kuamkia leo huko Tabata na hakuna mtu anayeweza kuvumilia maovu haya yanaofanywa na watu wasiokuwa na utu. Leo saa 12 asubuhi hospitali ya taifa Muhimbili imempokea mgonjwa anayeitwa Mussa Shabani(42) akiwa na shoka iliyonasa kichwani
(kama picha inavyooneka hapo chini).
Bwana Mussa ni mlinzi katika nyumba ya Joseph Mwakyusa huko Tabata. Majambazi yalipofika nyumbani kwa bawana
Mwakyusa yalimjeruhi
kwa shoka bwana mussa na, wakati majambazi yaliyovamia nyumba ya Mwakyusa yakiendelea kufungua spea za gari aina ya Toyota verosa. kwa bahati nzuri bwana Mwakyusa alishtuka
na ndipo
majambazi hayo yalipokimbia na kutoweka yakimuacha mussa katika hali mbaya na shoka ikiwa imenasa kichwani.
Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa
mahututi. bwana.
Jumaa Almasi afisa uhusiano mkuu wa MOI amethibitisha tukio hilo na kusema ''Ni kweli bwana Mussa amepokelewa hapa MOI akiwa na shoka iliyonasia
kichwani mwake lakini madaktari wamemfanyia upasuaji na kuitoa na sasa hivi yupo chumba cha wagonjwa mahututi''
Picha na maelezo kwa hisani ya FULL SHANGWE
Eeee Mwenyezi Mungu tunusuru, maumivu makali kiasi gani anayapata maskini, huu unyama utaisha lini jamani !!! inasikitisha sana !! ila umasikini ndio unachangia yote haya !!!
ReplyDeleteeeee mungu
ReplyDeleteHuu ni unyama uliyopita kiasi, tumnaomba vyombo vyote vya habari na Blog zionyeshe hizi picha ili vyombo vyote vya kidini na kiserekali vikemee vitendo hivi vya kikatili.
ReplyDeleteHuyu mtu anafayiwa hivi kisa alikuwa kazini anajitafutia riziki yake na familia yake. this is bull shit kumfanyia mwanadamu mwenzako vitendo kama hivi just because of a spare tire, ambayo bei yake for used hata dola 20 inaweza isifike. lakini angalia serikali itatumia milioni ngapi kwa matibabu na madaktari all that kwa ajili ya mtu hataki kufanya kazi anataka kuiba less that $20 dollas.
Watanzania tunaenda wapi, ni lini tutakuwa civilized?
Mashehe na wachungaji tusaidieni tafadhali, maadili hakuna kabisa, tunakuwa kama wanyama jamani? Alaaa