Baada ya kupewa mwaliko wa kutoa huduma ya neno la Mungu katika mkutano wa Injili mkoani Mbeya na kushindwa kufika kwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili Bi Rose Muhando, Pichani juu ni Bwana Riziki Mwakapugi akionesha stakabadhi za malipo ya benki(Pay in slip) ya shilingi milioni mbili nalaki tano zilizotumwa kwenye akaunti ya Mwimbaji huyo, kupitia benki ya Barclays. Mkutano huo wa injili ulioanza Novemba 18 hadi 20, mwaka huu uliandaliwa na kanisa la Bethel Miracle Centre(BMC), Kituo cha Mbinguni lililopo eneo la Soweto jijini Mbeya.
Jengo la Kanisa la Bethel Miracle Centre(BMC), Kituo cha Mbinguni lililopo eneo la Soweto jijini Mbeya, ambalo lilitoa mwaliko kwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Bi. Rose Muhando, na kushindwa kufika licha ya kulipwa fedha taslimu shilingi milioni Mbili na nusu alizokuwa akizihitaji ili aweze kuhudhuria.
Moja ya mabango yaliyotapakaa jiji zima likionesha muda, siku na mahali Mkutano wa injili utakapofanyika pamoja na wasanii wa nyimbo za Injili watakaotoa huduma ya neno la Mungu kupitia uimbaji, akiwemo Bi Rose Muhando, ambaye hakuweza kufika licha ya kuingiziwa kwenye akaunti yake shilingi milioni mbili na nusu alizokuwa akizihitaji ili aweze kuhudhuria.
Picha na Mbeya Yetu Blog
Rose Muhando naona hii tabia ya kuingia mtini imeshamiri. this year alialikwa America akaingia mtini baada ya kupokea down payment....hafai!
ReplyDeletekusema kweli inasikitisha sana kuona Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka Tanzania Wanavyoimba na Kumsifu Mungu huku wakitoa na MACHOZI lakini Wanatanguliza PESA MBELE!! Siyo Rose Muhando peke yake wako wengi tu. Kuna Waimbaji Kina Dada Watatu akiwemo Upendo Nkone na wengine Wawili waliokuja America mwezi October ilikuwa ni Kudai Pesa kila Kunapokucha bila ya kumuogopa Mungu wao. Jamani Fanyeni Kazi ya Mungu ili Mjiwekee Hazina yenu ya Mbinguni Msifanye kazi ya Mungu na Utapeli Juu!!
ReplyDelete