Thursday, March 1, 2012

SHULE YA WAMA(WANAWAKE NA MAENDELEO) WAPATIWA MSAADA WA BASI LA SHULE, VITABU NA VIATU

Mjasiriamali Loveness Mamuya akisoma barua toka kwa Mama Salma Kikwete.
Akikabidhiwa Basi dogo la shule
Wanafunzi wakiimba wimbo wa Taifa,shule ya WAMA (Wanawake na Maendeleo) ni shule iliyofunguliwa na Mama Salma Kikwete Jiji Dar kwa ajili ya kusaidia Wanafunzi wasiokua na uwezo kupata elimu, makabidhiano ya Basi hilo yalifanyika Jumanne Feb 28, New Jersey Nchini Marekani
Denise Lowe, Mkuu wa Shule ya Asbury Park, New Jersey akimueleza jambo Loveness Mamuya ambae alimuakilisha Mama Salma Kikwete na kumuagiza ahakikishe msaada uliotolewa na shule hiyo unawafikia walengwa.
Loveness Mamuya akitembelea moja ya madarasa ya shule hiyo.
Wanafunzi na Walimu wakimsikiliza Loveness Mamuya aliyesoma Barua kutoka kwa Mama Salma Kikwete.

      .Loveness Mamuya (wa pili toka kulia) akiwa na Shabani Mseba ( wa pili toka kushoto) wakipata picha ya pamoja na Waalimu wa shule hiyo.
Loveness Mamuya (kati) akiwa na Shabani Mseba (kulia) wakiwa na mmoja ya Walimu wa shule hiyo.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Asbury waliohudhulia makabidhiano ya msaada kwa shule ya WAMA wakipata picha ya pamoja na wawakilishi wa Mama Slama Kikwete Loveness Mamuya na kiongozi wa jumuiya ya wa Watanzania New York, Shabani Mseba.
Lovenes Mamuya na Shabani Mseba wakipata picha ya pamoja na Walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
 
Lovenes Mamuya na Shabani Mseba wakipata picha ya pamoja na Walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
Wanafunzi wakipata picha ya pamoja na wawakilishi wa Mama Salma Kikwete kwenye Bus walilotoa msaada kwa WAMA lenye uwezo wa kubeba Wanafunzi 50.
Kwa picha zaidi Bofya Read More
MABOX YALIYOJAZWA VITABU VITAKAVYOWEZA KUWASAIDIA WANAFUNZI WA SHULE YA WAMA.

BAADHI YA VITABU
WANAFUNZI WAKIKABIDHI VIATU KWA MAMUYA NA SHABAN KUTOKA KWA MKURUGENZI WA NEW JERSEY NATURAL GAS.

23 comments:

  1. Ok sasa wanasaidia wamerekani badala ya kusaidia Tanzania watoto ambao wanashida Mimi sielewi hii kitu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Taarifa zote zinajieleza kabisa, ni msaada unaokwenda Tanzania, shule ya WAMA. Dada Loveness Mamuya na Kaka Shaban Mseba, wamepokea hiyo misaada kwa niaba ya Mama Salma Kikwete, ili wahakikishe kuwa inafika kwa walengwa.

      Delete
  2. Big up dada loveness Naamini kabisa vitu vitafika salama na zaidi vitakuja kazi nzuri unayoifanya kwa wananchi wako moyo wako wa kusaidia uwendelee kujituma kwa moyo mmoja bila kujali majungu wala fitina ubarikiwe na kila ufanyalo !!

    ReplyDelete
  3. Labda nimueleweshe hapo juu ni kwamba msahada ni kutoka marekeni ni vitabu na viatu na bus la watoto wa shule la kuwasaidia shule inaitwa wama ni yaya mama kikwete na mama anafanya kazi nzuri sana ya kujitolelea kwa kuwa yeye ni mwalimu wa shule basi anashule zake nne zipo dar es saalam nini ambacho ujaelewa mdau?? uliza kitu kama haujui kuliza sio ujinga ....!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio shule za Mama kikwete bali mwanzilishi wa WAMA ni Mama Kikwete. In short Mama Kikwete kama first lady ametumia nafasi yake kupata misaada kutoka balozi mbalimbali kuanzisha project aliyoiona inafaa kusaidia Watanzania. Ni kama vile Mama Anna Mkapa na mfuko wa fursa sawa kwa wote. Although wao ni waanzilishi lakini kuna bodi, wajumbe etc na "outside watchers wanaoangalia fedha zile zinatumikaje". Sio business ya familia; so sidhani kama ni lugha sahihi kusema ni shule za mama Kikwete.

      Delete
  4. Loveness ni mwakilishi wa Mama Kikwete? Ubalozi wetu uko wapi kuhakikisha vitu vinafika Tanzania kwa wahusika?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante anon 7.24am namimi nimejiuliza hivyo hivyo. Je huyu Loveness yeye anafanyakazi WAMA? Kama ndio mbona hawajaandika yeye kama mwakilishi wa WAMA na sio wa Salma Kikwete. Ingawaje Salma Kikwete ndio mwanzilishi lakini WAMA ina-bodi na wajumbe etc so sijaelewa kama tatizo ni uandishi wa hii habari au tatizo ni zaidi ya hapo. Job true true!

      Delete
  5. Jambo kubwa hapa ni hilo Bus. Mabasi ya aina hii kuyamaintain kwetu Tanzania ni matatizo. Ni vyema Dada Loveness akalielewa hilo. Naamini litakuwa ni mzigo. Model hizi Afrika inakuwa shida tupu. Kwanza injini nyuma na heat ya Bongo havikubaliani kabisa. Kitu kingine spare parts. Tafadhalini musishabikie kupokea bus bila ya kujua matatizo yaliyoko mbeleni.

    ReplyDelete
  6. Kwanza naomba muelewe hii Wama ni Wanawake na maendeleo na sio serekali wala ubalozi hausiki ...Na Loveness ni kati wajumbe wa wama na mpenda maendeleo sasa sioni sababu ya wewe kukasirika kwa nini amewakilisha kwanza yeye amefanya kazi kubwa sana kutupatia hii misaada na kuelekeza nyumbani la angeweza kupeleka popote wewe kama ni mtanzania unatakiwa ujitahidi kutafuta misahada na mpeleke jusaidia nyumbani kama alivyofanya dada loveness badala ya kuandika kwanza kila mtanzania akijitahidi kutafuta misaada kama hii basi tungeweza kufika mbali kwa kweli .Tupendandane tusaidiane na tuache kukosoana bila sababu !!! Wama wanapokea misaada yoyote bila kipingamizi

    ReplyDelete
  7. Kwa kweli Leo watanzania nimeamini mna chuki binafsi Hamna maana wewe luka ulitakiwa hizi comment wala usiziweke ni aibu kubwa sana hawa wanouliza ni wajinga wamwisho msaada hawajui hata ulipotoka wao ni vuvuzella kama lovenes ndio alitafuta msaada huyo mnajuwaje ?wacheni ujinga wenu tafuteni kazi za kufanya mbona akisaidia misibani sijaona mkasema yeye sio mtu wa ubalozini ??wacheni midomo yenu mshindweee

    ReplyDelete
  8. Maana na kazi za ubalozi ni kazi za serekali na wala sio za chama chochote mtambue hilo watanzania kazi nzuri dada lovens tanzania itajengwa na kila mwana nchi na kila mwenye uwezo ni kazi yako wewe kuisadia nchi na wala sio serikali nawaombeni sana mjue hilo Tanzania ni nchi ya maskin duniani tuangaike tufute umaskini na sio turudishane nyuma na maneno ushirikiano ni jambo la busara sana .Tanzania nchi ya upendo mbona sioni upendo ??tubadilike natushikane!

    ReplyDelete
  9. Bandugu umoja ni nguvu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kazi ya Luka ni kuchapisha maoni ya watu mbalimbali bila ubaguzi, ili mradi hayajatukana mtu. Kama wewe yamekuumiza..pole. Luka asilaumiwe, yeye ni mpashaji/mchapaji wa taarifa. Tumia nguvu ya hoja kupingana na hoja zilizopo kuhusu UHALALI wa wewe 'dada' Loveness kumwakilisha mama Kikwete na Serikali ya Tanzania.Mambo ya michango misibani, harusini hayahusu jamani.

      Delete
  10. Jamani nimeamini kweli waTZ wengi ni mbumbumbu!hata kiswahili pia hamuelewi?na hapa tuko mamtoni kweli hii balaa,sasa kiingereza inakuaje wenzangu akina MAIMUNA?habari inajieleza kabisa dada Loveness alikwenda kupokea misaada inayokwenda bongo kusaidia watoto wa WAMA!na yeye akiwa ni mwakilishi wa Salma kikwete!sasa hiyo ubalozini imeingiaje?hivi ni vitu viwili tofauti jamaniiii!acheni wivu!maanake kama vile mshaanza kumkosoa.Kazi nzuri dada Loveness!mimi ndio nakupendea hapo,kaza buti mama.Mbona vitu vingine anajitolea anafanya hamsemi lakini hiki mnaongea,hebu acheni wivu,tuwe na wivu wa maendeleo,hapo hana hata cheo kaenda kuwakilisha tu! mnaongea je angekua nacho?.

    ReplyDelete
  11. Hivi hapa ni tatizo ni nini ??hii mnaonyesha wazi mlivyo na wivu dada upo juu bwana Tunataka watu Kama wewe katika jamiii yetu naomba achana na watu Kama hawa waSio na maana move on my sister kwanza nani hapa alishawahi kusaidia nyumbani hata mutumba ?? Nakuaminia sister unaweza sio mchezo Mtu wangu wachana na waswahili hawana wema

    ReplyDelete
  12. Wabongo tunapenda sana kukosoa wenzetu, je wewe ukipewa jukumu la kwenda kumuwakilisha mama kikwete unaweza? maybe hata hiyo nauli ya kukufikisha huko New York ingekuwa ngumu kuipata. Don't hate, congratulate.... and if you can't beat them, join them. Tuacheni chuki binafsi tujifunze kuwa na roho safi kama dada Loveness, wengi wetu hatuna hiyo confidence na ability. Hata kwenda hapo kwenye hiyo shule ingekuwa migogoro maana "ze maza ze mama Kikwete is kutumaring me to here,blah blah". Nyie mnaolalama mnapenda kuona watu wako kwenye level yenu tu, wakijituma kidogo tu misuli inawatoka. Tukue jamani this is 2012 tumeshazeeka.

    ReplyDelete
  13. Soma kabla hamjauliza swali nini hapo hamuelewi ?? AMA luka unaagenda ya Siri ?? Muacheni kumchafulia sister wabongo nuksi kweli duu hatari wachai kweli mbona haukubali comment Leo vipi AMA ndio na wewe walewale

    ReplyDelete
  14. Wewe anonymous wa march 2,10.13pm,acha kuhadaika bwana,dada Loveness kalipiwa nauli,kalipiwa hoteli,usafiri chakula bureeeee!na malupulupu juu,kwahiyo acha kupiga mayowe kua eti mtu akiambiwa aende yeye atakosa hata nauli,yeye ni mjumbe ametumwa kwahiyo ana rights zote za kuhudumiwa na waliomtuma,unachekesha.Si unapanda mchina tu hapa chinatown!!!!!!haaaaaaa!haaaaaaa!haaaaa!Hivi kwanza mjadala huu wa dada Loveness jamani uishe,mbona kuna vitu vingi sana vya kujadili na kutoa comment hapa?.Tuelimike jamani baada ya miaka 50 ya uhuru bado tuko hivihivi!.

    ReplyDelete
  15. Nimesoma comment zoooooteeeee hapa lakini nimeona asilimia kubwa ya watu wanamuunga mkono na kumpongeza Loveness.Hakuna ubishi kwa hilo,tunaomba na mjasiriamali mwingine aige mfano huu,watu kama hawa ndio tunaowahitaji katika jamii yetu ya umasikini,fungeni mjadala mwacheni dada wa watu,Alamsiki.

    ReplyDelete
  16. Jamani mimi nimesoma kwa makini sana hii issue,sio dada Loveness ndio aliyefanya mpaka misaada ikatolewa ila mama kikwete ndio amepewa hiyo misaada baada ya kuomba kutokana hapa marekani ikasaidie shule ya WAMA ambayo anaisimamia mama kikwete.Kwakua yeye labda kwa ajili ya kutingwa na kazi au nini ndio akamchagua dada Loveness amwakilishe pale!lakini swali nalojiuliza mimi na watu wengine pengine ni kwamba kwa nini yeye?mbona sio mjumbe wa WAMA wala mtu yeyote kwenye chama wala serekali,na hatujawahi kumsikia yuko kwenye chama chama chochote kila wala kuongoza chochote.Mmmh hebu tufafanulieni jamani,kuuliza sio ujinga.

    ReplyDelete
  17. Watanzania tuna kazi kubwa sana mbeleni na tusipokuwa na umoja nchi yetu itazidi kudidimia. Hongera dada Loveness kwa kuwa mfano katika kuleta maendeleo ya nchi yetu. Leo nilikuwa naangalia kipindi cha 20/20 kwenye channel ya ABC inasikitisha sana kuona maisha ya walemavu wa ngozi (albino) yalivyo nyumbani. Walemavu hawa wanavyowindwa na kuuawa kwa imani za ushirikina na mpaka mmoja wao amekuja kuomba Congress iwasaidie kuwalinda. Sijui serikali yetu inafanya nini kuhusu jambo hili mpaka Congress iweke sheria za kulinda albinos Tanzania!!! Kuna maeneo mengi Tanzania ambayo tukishirikiana tutaleta mabadiliko makubwa. Asante dada Loveness kwa kuwa mfano. Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake