ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 15, 2014

MREJESHO WA TAMKO LA WACHUNGAJI KUHUSU UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA WASHINGTON DC,MARYLAND NA VIRGINIA ULIOFANYIKA SEPTEMBA 9,2014

kkKwanza wanajumuiya wenzangu napenda kuchukua fursa hii kwa uangalifu kujibu hizi tuhuma za upotoshaji kutoka kwa wachungaji kuhusu uchaguzi wa jumuiya ya DMV. Inasikitisha sana kuona wachungaji wetu(Mathayo Malekela, Ferdinand Shideko, Mellchizedek Maturlu, John Kadyollo, Peter Igogo na John Mbata) kwa makusudi kabisa  wameamua kuigawa jumuiya yetu ya DMV kwa sababu ya matakwa yao binafsi kwa kuandika waraka kwenda kwa Balozi wetu MulaMula kwa kutumia facebook na blogu!!!. Naomba tuangalie madai yao hapo chini kama ifuatavyo!!!!:

              1.YALIYOJITOKEZA KABLA YA UCHAGUZI

A)Mgombea mmoja kupewa nafasi ya kuzungumza mbele ya Rais Jakaya Kikwete

>Nafikiri hawa wachungaji hata homework yao hawajaifanya vizuri, sababu kwanza ujio wa rais Kikwete hauhusiani chochote na uchaguzi wala tume ya uchaguzi DMV. Wamesahau kwamba bado tulikuwa na Rais wa jumuiya ya DMV na kutokana na protokali lazima azungumze. Sasa mlitaka na Libe naye azungumze kama nani. Dhana hii haina ukweli wowote na ni upotoshaji wa makusudi kutoka kwa hawa wachungaji.

2.WAPIGA KURA HAWAKUWA NA KITAMBULISHO CHA KUPIGA KURA

>Nafikiri wachungaji walikuwa nyuma kufuatilia utaratibu ambao tume ya uchaguzi ilitangaza siku tatu kabla ya uchaguzi. Kwanza tume ya uchaguzi ilitoa majina ya wanachama ambao wamelipa ada ya kujiunga na jumuiya na kusema ili uweze kupiga kura inabidi uwe na kitambulisho chako(state ID/Driver license) kinaonyesha mahali unapoishi. Na siku ya uchaguzi ili kufanikisha zoezi hili wapiga kura wote tulihakikiwa majina yetu mara tatu kabla hujapewa karatasi ya kupigia kura. Wakati wamesahau kwamba wao walikuja na waumini wao ambao hawakuwa hata na kitambulisho  wala passport na hao wachungaji wakawaomba wasimamizi wanaohakiki majina kwamba wanafahamu na ni waumini wao, kwa kuamini kauli zao waumini wao waliruhusiwa kupiga kura bila kitambulisho.

3.UANDIKISHAJI WA KUPIGA KURA ULIKUWA KIMAKOSA

>Kwanza tuweke mambo bayana, nani alikuwa anachukua fedha za kuandikisha wapiga kura? Jibu ni wakala wa kila mpiga kura na ilikubalika na tume ya uchaguzi kwamba wakala anachukua ada ya mwanajumuiya na kuandikisha jina lake katika orodha ya kitabu cha kupigia kura na kuiwakilisha kwenye tume. Nafikiri hapa inaonyesha jinsi gani hata utaratibu hawa wachungaji hawaujui sababu
hawakuwa ndani ya jumuiya(hawakuwa wanachama hai na lengo lao lilikuwa kuja kupiga kura tu)!!!

4.WAKATI WA UCHAGUZI HAPAKUWA NA ALAMA YA WINO KUONYESHA UMEPIGA KURA

>Hivi kweli mnajua ni utaratibu gani tume ilijiwekea(Utaratibu ulikuwa ukishatoa jina lako na baada ya kuhakikiwa lilikuwa linafutwa kwa kalamu kwa mchoro wa mstari mmoja ili kuepusha  udanganyifu. Kujaribu kulinganisha na wino haina uzito wowote zote ni njia za kufanikisha chaguzi. Kama hapa Marekani tunapowachagua viongozi wa serikali tukipiga kura tunapewa sticker hatutumii wino.

5.MAKUNDI KUPIGA KAMPENI NJE YA UKUMBI SIKU YA UCHAGUZI!!!!

>Kwa kweli inasikitisha sana kuona hawa wachungaji hata hawajui utaratibu wetu wa kupiga kura hapa DMV. Katiba ya jumuiya haimkatazi mgombea yeyote kufanya hivyo. Inaruhusiwa kufanya kampeni mpaka mwisho wa kupiga kura,nafikiri hawa wachungaji wanataka kuchanganya mambo ya siasa na jumuiya sababu hatufanyi kampeni za kisiasa hapa.

6.MASANDUKU YALIKUWA NA GIZA

>Kwanza masanduku yote yaliletwa na mmoja wa wakala wa aliyeshindwa urais na akayafungua kila mtu aliyekuwepo pale akaona hakuna kitu ndani yake, na kila mgombea akaweka wakala wake pamoja na tume ya uchaguzi kulinda masanduku ya kupigia  kura. Hiyo sababu kwamba yalikuwa na giza ni mawazo taka na hayana mantiki yoyote. Na baada ya kura zote kumalizika kupigwa kila wakala wa mgombea alikuwa anahesabu  kura za mgombea anayemwakilisha.

7.BAADA YA UCHAGUZI KUNA KURA ZA ZIADA 9.

>Mnajiuliza zimetoka wapi? Hebu tumuulize wakala wa Libe ambaye ndiye alipewa jukumu la kutoa karatasi za kupiga kura nini hasa kimetokea?! Au tuwaulizeni nyie wachungaji ambao mnasema mnatetea haki, wale waumini wenu ambao majina yao hayakuwa katika orodha ya wapiga kura wala hawakuwa na vitambulisho na sababu ya ushawishi wenu wakaruhusiwa kupiga kura!!! Hao hamuoni hilo kuwa ni tatizo, ila mnataka kuwapotosha wana jumuiya kwa dhana yenu potofu sababu hamkufanikiwa mlichokipanga.

UKWELI  KUHUSU NYIE NA ITIKADI ZENU

Hebu wana DMV turudi nyuma kuhusu hawa wachungaji; kama tunakumbuka vizuri hawa wachungaji  walianzisha kanisa moja wakiwa wote kwa pamoja. Baada ya muda mfupi tu kwa sababu ya tamaa zao binafsi wakavunja kanisa lile na kila mmoja akaja na kanisa lake. Waumini ambao ni kondoo ambao wanahitaji mchungaji wakaachwa bila mwangalizi na malisho. Hauhitaji kuwa genius kugundua hawa wachungaji na itikadi zao za kibinafsi. Sasa mnazungumzia umoja!!! Umoja upi huo wakati nyinyi wenyewe mmeshindwa kuwa wamoja. Nendeni kwanza mkaungane liwe kanisa moja la kiswahili na kuwakusanya watanzania waje wasali pamoja na hapo anza kuzungumzia Umoja na Mshikamano.    

KWA MANUFAA YENU KABLA HUJATOA KIJITI KATIKA JICHO LA MWENZIO TOA KWANZA BORITI KATIKA JICHO LAKO. ACHENI UNAFIKI NA MSITUHARIBIE JUMUIYA YETU KAMA MLIVYOHARIBU MAKANISA YENU.

Wenu,
MwanaDMV.    

9 comments:

Anonymous said...

Ndugu aliyechangia sasa umenifurahisha sana kwani wa Chunga ji wanatakiwa kurudisha kondoo zizini na siyo kuharibu hapa udini umetembezwa wachungaji kaa chonjo muda wenu mnaupoteza kwa hili badala ya kuunganisha waumini mnaleta watu kupiga kura halafu msijue kura zaidi zimetoka wapi Halloooooooo!!!!!! Mmekoroga zege mlinywe hilo!!!!!

Anonymous said...

Hawa wachungaji kama kweli wanapenda umoja, kwanini waligombana na kusambaratika kila mmoja wao akaenda kuanzisha kanisa lake?. Kwanini wasiwe na kanisa moja kama wenzao wakatoliki? Hawa wote wamezamia hapa DMV na kutelekeza familia zao Afrika. Kama wanapenda umoja, kwanini wanaishi mbali na wake na watoto wao? Hakuna hata mmoja mwenye makaratasi kati yao. Kama wanapenda haki na uhalali kwanini walidanganya wakati wa kuomba viza? Kama wanapenda haki, kwanini baadhi yao wanatumia majina ya watu kufanyia kazi? Hawa wote walikuwa siyo wanachama wa jumuiya, anyway. Nani kawatuma leo waongelee jumuiya?

Anonymous said...

Hivi mnatania sio nani aliwapa hao UCHUNGAJI??? Hao ndio wale waliotumwa kutuharibu na kututenga.. Mungu amewaumbua mwenendo wao... Kazi ya SHETANI ni kugombabisha watu sasa hawa wanaojiita wachungaji wanatugombanisha tu...

Anonymous said...

Kama kweli unataka kujibu hoja kwa nini ufiche jina lako.madai yote yaliyosemwa na wachungaji ni kweli.idd hakuwa raisi wa dmv tangu feb alitakiwa kuwa na election SINCE feb kwa makusudi ukachelewesha uchaguzi.kikatiba wewe idd hukuwa raisi halali tangu feb.

Anonymous said...

Inasikitisha kuona watu wanaojulikana kama viongoziwa dini ndio wa mwanzo kusimamisha fitina katka jamii iliyotulia. Mnarudia historia ile ile mlioifanyia Tanzania wakati wa Uhuru. Waisilamu walipigania Uhuru, huku nyinyi mmekaa pembeni na hata kushirikiana na wakoloni, baada ya uhuru, mkaingia kuivuruga nchi kwa udini. Leo hii, mnaongozwa na Muisilamu, chuki zimewajaa. Wacheni ufukara wa fikra.

Muogopeni Mungu,kwa kujizuia na chuki na njaa.

Anonymous said...

Mbona wewe umeficha jina lako?

Anonymous said...

Wachugaji wenyewe hawa tunaopishana kwenye madangulo? Au mnataka nitaje mmoja baada ya mmoja na wapi tunako pishana? Come on wachungaji

Anonymous said...

Well mimi na comments tu,lakini wewe idd unaendika article na kuwashutumu wachungaji ni busara kuweka jina na signature yako, usijifiche,na ukiona unajifisha maana yake unaandika pumba.first of all huna confidence ya kuandika jina lako wote wanafiki

Anonymous said...

Ningemshauri Libe kuanzisha jumuiya nyingine mpya ya wana-DMV.Hii itatoa fursa mpya ya sisi sote(DMV) kutekeleza VISION mpya na siyo hiyo ya akina Sandali na udini wake.