Advertisements

Saturday, April 27, 2024

RUVUMA:JESHI LA POLISI WAMTIA MBARONI MTUHUMIWA WA WIZI WA VIFAA NDANI YA MAGARINI HALFA MINJA MKAZI WA SANAWALI JIJI LA ARUSHA


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma Kamishina msaidizi Mwandamizi Marco Chilya,akionyesha baadhi ya kompyuta Mpakato(Laptop)zilizokamatwa na Polisi kutoka kwa kinara wa wizi ya vifaa vya ndani ya magari mkazi wa Mtaa wa Sanawali Jijini Arusha Halfa Minja,kukatamtwa kwa mtuhumiwa huyo kutokana na operesheni zinazoendelea kufanywa na Jeshi hilo katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Kamishina msaidizi Mwandamizi Marco Chilya,akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jana wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watu mbalimbali wanaojihusisha na vitendo vya uharifu mkoani humo.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma Kamishina msaidizi mwandamizi Marco Chilya,akiwaonyesha Waandishi wa Habari(hawapo pichani)baadhi ya milipuko(baruti) aina ya Super Powder 90 zenye vipande 12 kila moja iliyokamatwa na Jeshi hilo kutoka kwa mkazi wa mtaa wa Hoa Hoa wilayani Mbinga Edmund Komba(34) ambaye alikutwa na Dazeni mbili za milipuko hiyo kinyume cha sheria

Na Mwandishi wetu Ruvuma
KAMANDA wa Jeshi la polisi mkoani Ruvuma Kamishina msaidizi Mwandamizi Marco Chilya amesema,wanawashikilia watu watatu akiwemo mkazi wa mtaa wa Sanawali Jijini Arusha Halfa Minja kinara wa wizi wa vifaa ndani ya magari mkoani humo.

SAKATA LA DKT KAWAMBWA: DIWANI MSTAAFU WEMBE, ASKARI MGAMBO MIKONONI MWA POLISI


JESHI la Polisi Mkoani Pwani limewtia mbaroni Diwani wa kata ya Kiromo Mstaafu Hassan Wembe na Askari Mgambo Abdallah Mgeni na baadae kupewa dhamana, kwa kosa la kumshambulia kwa maneno makali, vitisho, dharau na kutishiwa kufungwa pingu Waziri na Mbunge Mstaafu Dkt Shukuru Kawambwa pamoja na Cathbert Enock Madondola huko Kitopeni, wilayani Bagamoyo.

Aidha watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo (pichani), alieleza kwamba tarehe 25 April mwaka huu kupitia mitandao ya kijamii ilionekana clip ikimwonesha Dkt. Kawambwa akishambuliwa kwa maneno na vitisho na kudhalilishwa , kufokewa na kutishiwa kufungwa pingu kama mhalifu hali iliyosababisha taharuki kubwa kwa jamii.

"Ukweli ni kuwa April 24 saa 8 mchana Dkt. Kawambwa na mtu mwingine Cathbert Madondola walishambuliwa kwa maneno, vitisho na kutishiwa kufungwa pingu na diwani Mstaafu kata ya Kiromo Hassan Wembe akiwa na askari mgambo Abdallah Mgeni."alifafanua Lutumo .

Vilevile Kamanda huyo, amemtaka mtu aliyechukua na kusambaza video ya Dkt. Kawambwa na Cathbert Madondola wakati wakishambuliwa kwa maneno makali na kutishiwa kufungwa pingu na diwani Mstaafu huyo Wembe ajisalimishe kituo cha polisi Bagamoyo mara moja.

KOMANDOO WA JWTZ WANOGESHA SHEREHE ZA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Askari wa Kikundi Maalum cha Komando cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akipita mbele ya jukwaa kuu na zana zake wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024
Askari wa Kikundi Maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akishuka kwenye Helikopta kwa ajili ya kwenda kuelezea namna mbalimbali za kwata na mapigano ya mjini wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
Askari wa Kikundi Maalum cha Komando cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionesha Maonesho mbalimbali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.
Askari wa Kikundi Maalum cha Komando cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionesha Maonesho mbalimbali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.

TANROADS YAWEKA KAMBI BARABARA YA MOROGORO- IRINGA KUZIBA MASHIMO MAENEO YALIYOHARIBIWA NA MVUA



Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro inaendelea na kazi ya kuziba mashimo na kukarabati barabara kuu ya Morogoro – Iringa ikiwemo katika eneo la Kobogwa lilipo katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo kumetokea shimo kubwa baada ya maji kupita pembezoni mwa Kalvati.
Akizungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa leo tarehe 26 Aprili 2024; Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe L. Kyamba amesema kuwa tayari Mkandarasi yupo eneo hilo akiendelea na kazi ambapo mpaka kufika leo usiku kazi hiyo utakuwa imemalizika.

"Mvua zimeendelea kunyesha bila kukatika na jitihada zinaendelea kufanyika kila siku, eneo hili ambalo limeleta taharuki katika barabara hii ya Mikumi. Mashimo yametokea juzi, tukayaziba kidharura lakini unapoziba kidharura mvua zikinyesha tena zinaondoa ule mchanga ambao tumeuweka kwa sababu kipindi hiki cha mvua huwezi kuziba na lami, lami haikubali kipindi cha mvua mpaka jua liwake" Amekaririwa Mhandisi Kyamba na kusisitiza kuwa
“Tunaendelea na kazi ya kuziba mashimo yote kwenye barabara hii kuanzia Msamvu - Mikumi hadi Iringa mpaka tuyamalize kutokana na mvua kubwa kila siku mashimo yanajitokeza juzi hapa kwenye hili Kalvati maji yamepita pembeni yametengeneza shimo kubwa hapa katikati tukaanza kuleta mitambo na nyenzo za kazi, kwa sasa barabara inapitika upande mmoja na upande mwingine kazi inaendelea’’

Friday, April 26, 2024

RAIS WA ZAMBIA HAKAINDE HICHILEMA AWASILI KWA SHEREHE ZA MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema tayari amewasili nchini kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania ambapo amepokelewa na Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde.





RAIS SAMIA AKIWA KWENYE SHEREHE ZA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa katika Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kushuka kwenye gari Maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024.

BUNGE LAPITISHA SH. TRILIONI 1.8 MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI 2024/2025



-95.28% kuelekezwa kwenye maendeleo
-Serikali kuja na Kanuni ya Uwajibikaji kwa wananchi Miradi ya Mafuta na Gesi Asilia
-Dkt. Biteko aagiza Halmashauri kupeleka fedha za Ushuru wa Huduma vijijini
-Masharti ufunguzi wa vituo vya CNG yarekebishwa kuvutia uwekezaji
-Kapinga atilia mkazo utekelezaji Nishati Safi ya Kupikia na CNG

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha shilingi Trilioni 1.8 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati katika mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo asilimia 95 ya bajeti hiyo imeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akijibu hoja mbalimbali za Wabunge ameeleza kuwa, ili wananchi wanaozunguka miradi ya Gesi Asilia na Mafuta wafaidike na rasilimali hiyo Serikali itapitisha kanuni itakayoongoza Miradi ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) ili kampuni ziweze kuwajibika ipasavyo kwa jamii.


Aidha, kuhusu ushuru wa huduma (service levy) unaotolewa na kampuni za Mafuta na Gesi kwa Halmashauri mbalimbali nchini, Dkt. Biteko ameagiza Halmashauri hizo zihakikishe kuwa sehemu ya fedha hizo zinarudi kwenye vijiji ambapo miradi inatekelezwa.

“Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati wasiliana na Katibu Mkuu TAMISEMI ili kuja na mpango wa utekelezaji wa service levy ili fedha zinazotolewa ziende pia kwenye maeneo ambapo miradi inatekelezwa, Rais ameshaeleza hataki kuona malalamiko sehemu ambapo Gesi inachimbwa, Service Levy na CSR sasa zitaanza kufanyiwa kazi kwa kasi kubwa.” Amesema Dkt. Biteko

SERIKALI YA MAREKANI YAZINDUA MPANGO VYA VYANDARUA VILIVYOTIWA DAWA ZANZIBAR


SERIKALI ya Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) wameungana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani na kutangaza kampeni ya usambazaji wa vyandarua vilivyowekwa dawa kwa Zanzibar yote.

Kwa mujibu wa Utafiti wa Viashiria vya Malaria Tanzania wa mwaka 2022, Zanzibar bado ina kiwango cha malaria chini ya asilimia moja kwa zaidi ya muongo mmoja.

Hiyo ni kutokana na mchango mkubwa kutoka serikali ya Marekani kupitia Mpango wa Rais wa Marekani wa mapambano dhidi ya malaria na ushirikiano na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwamba hivi karibuni idadi hii iliongozeka.
Akizungumza kuhusu Mpango huo Waziri wa Afya Zanzibar Dk.Nassor Ahmed Mazuri amesema pamoja na kupungua kwa namba ya wagonjwa wa malaria Zanzibar, amegundua hivi karibuni kuna baadhi ya wilaya zimeshuhudia ongezeko la wagonjwa wa malaria.

" Hili halikubaliki Zanzibar, naomba hatua zote zichukuliwe kudhibiti ugonjwa ya malaria kwa kushirikisha sekta zote zinazohusika” amesema Dk Mazrui.

RAIS DKT. MWINYI AKOSHWA NA MDAHALO WA WANAWAKE NA MUUNGANO, AIPONGEZA UWT.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwasilimia Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) walipowasili katika ukumbi wa mkutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kulifungua Kongamano la Wanawake na Muungano lililofanyika 25-4-2024.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Kongamano la Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika 25-4-2024 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano hilo.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa na Wake wa Viongozi wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifungua Kongamano hilo lililofanyika 25-4-2024 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Kongamano na Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishingilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam 25-4-2024.(Picha na Ikulu)

MISA YA KUMBUKUMBU YA BISHOP FRANSISCA GACHUMA, SILVER SPRING, MARYLAND

 Picha za siku ya kumbukumbu ya Bishop Fransisca Gachuma iliyofanyika siku ya Jumapili April 21, 2024 katika hotel ya Double Tree iliyopo Silver Spring, Maryland, misa hiyo iliyoandaliwa na watoto wa marehemu Gatty na Eddah ilihudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wengine wakitoka majimbo nje ya DMV huku Bishop Dr. Livingston Banjangala akiongoza misa hiyo






RAIS RUTTO AWASILI NCHINI KWA SHEREHE ZA MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh. William Samoei Rutto akipokewa na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde wakati alipowasili nchini Tanzania kwa ajili ya kushiriki katika maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Thursday, April 25, 2024

TAADHARI IWE NGUZO KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA NYINGI - KAMSAMBA


Na Issa Mwadangala
Wananchi wa Kata Mkulwa Tarafa ya Kamsamba Wilaya ya Momba Mkoani Songwe wametakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua nyingi zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali wilayani humo

Rai hiyo imetolewa Aprili 25,2024 na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Momba Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Kennedy Msukwa wakati alipokuwa akitoa elimu juu ya madhara ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali wilayani humo.

SSP Msukwa amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kuongeza umakini katika malezi ya watoto hasa katika kipindi hiki cha mvua nyingi zinazoendelea kunyesha ikiwa ni pamoja na kuwakataza kucheza michezo hatarishi kama kucheza na kuogelea kwenye maji yaliotuama (madimbwi) mabwawa na mito.
“Wazazi na walezi shughuli za kutafuta nguvu ya tumbo ziende sambamba na malezi ya watoto msiwaache watoto wajilee wenyewe kitendo ambacho kinapelekea watoto kusombwa na maji au kudumbukia kwenye mabwawa, mito na visimani kitendo hiki kinapunguza kizazi cha kesho ambacho ni hazina kwa taifa letu” alisema SSP Msukwa.

“Wavuvi mnatakiwa kufuata sharia na utaratibu wa shughuli zenu za kila siku ikiwa ni pamoja na kufanya uvuvi salama pia kuangalia hali ya hewa kabla ya kuingia kwenye shughuli zenu ili kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kuepukika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu pindi muonapo au mfanyiwapo kwa Jeshi la Polisi ili zishughulikiwe kwa haraka ili maeneo yenu yaendelee kuwa salama” alisisitiza SSP Msukwa.

PSPTB YAWAFIKIA WANACHUO WA CHUO CHA BAHARI DAR ES SALAAM



Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kilichopo jijini Dar es Salaam.

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo Wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) hii ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu kwa umma hasa kwenye vyuo vinavyotoa masomo ya Ununuzi na Ugavi.
Akizungumza na Michuzi Blog, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee amesema Bodi hiyo imeendelea kuwapa mafunzo Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wanaochukua kozi hiyo ya Ununuzi na Ugavi kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi, Usajili kwa njia ya mtandao pamoja na maadili na miiko ya taaluma hiyo.

Naye, Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi katika Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Jonnes Lugoye ametoa shukrani kwa wafanyakazi wa PSPTB kwa kuweza kufika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi.
Kaimu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi - DMI, Jonnes Lugoye akiwakaribisha wageni kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) walipofoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Bodi hiyo.

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AMEWAAGIZA UCSAF KUENDELEA KUSIMAMIA UJENZI WA MINARA YA MAWASILIANO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye mara baada ya hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja watumishi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mara baada ya kuzindua jengo la Taasisi hiyo lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) lililopo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma. Tarehe 25 Aprili 2024.

TUMIENI UZOEFU KUHARAKISHA MABADILIKO - BALOZI KUSILUKA


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka akiongea na Mabalozi katika warsha ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika mjini Kibaha, Pwani.
Kutoka Kushoto; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses, Naibu Waziri Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato wakifuatilia warsha ya Mabalozi ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere mjini Kibaha, Pwani.

Mabalozi wamehimizwa kutumia taaluma, uzoefu na ujuzi tofauti waliokuwa nao kuharakisha mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolewa  Aprili 23, 2024 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka wakati anaongea na Mabalozi katika warsha ya siku 4 ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika mjini Kibaha tokea tarehe 21 Aprili 2024.

"Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mmebarikiwa kuwa na watu wenye taaluma tofauti na wenye historia ya sekta tofauti, tumieni fursa yenu hii kumsadia Mwanadiplomasia namba moja, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewarahisishia kazi yenu kwa kuitekeleza diplomasia kwa vitendo", Balozi kusiluka alisema.

WAKUU WA SHULE, MADEREVA ZINGATIENI USALAMA WA WANAFUNZI KIPINDI CHA MVUA - MAJALIWA



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa shule na madereva wa mabasi yanayotoa huduma za usafiri kwa wanafunzi wajiridhishe kuhusu njia wanazopita ili kuhakikisha kunakuwepo na usalama wa wanafunzi wanaowabeba katika vyombo vya usafiri.

“Wazazi, Walezi na Jamii ya Watanzania kwa ujumla tushiriki kikamilifu katika kuhakikisha usalama wa wanafunzi wanapokwenda na kurudi Shuleni wakati wote hususan katika kipindi cha mvua.”

Kadhalika amesema kwa kuwa Serikali imetoa maelekezo ya kufunga shule zilizoathiriwa na mafuriko, halmashauri na wamiliki wa shule zisizo za Serikali waweke utaratibu wa kufidia muda wa vipindi ili kukamilisha kalenda ya muhula kama ilivyopangwa.

Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Aprili 25, 2024) wakati akitoa taarifa ya serikali kuhusu changamoto za hali ya hewa bungeni jijini Dodoma.

Pia, amezitaka Taasisi za Serikali ziendelee, kukabiliana na maafa kwa kushirikiana na wadau kutekeleza majukumu yaliyoanishwa katika Mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na Madhara ya El-Nino pamoja na mipango ya kisekta ili kuzuia na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

“Kamati za Maafa za Wilaya na Mikoa ziendelee kuchukua hatua stahiki ikiwemo kutoa tahadhari kwa wananchi na kusaidia wananchi kwa wakati pindi maafa yanapojitokeza.”

RC TANGA ATOA NENO KWA WANUNUZI WA ZAO LA MWANI


Mkuu wa Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea wakulima wa zao hilo katika Mtaa wa Sahare Kijijini Kata ya Mzingani Jijini Tanga ambao pia alizungumza na wakulima wa zao hilo kwenye wilaya za Tanga,Mkinga ,Muheza na Pangani ikiwa ni kuelekea Shamrashamra za kuelekea miaka 60 ya Muungano.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akitembea kuelekea baharini kuangalia kilimo cha Mwani wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wakulima hao
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akitoka kukagua zao la Mwani wakati wa ziara yake
Afisa Mfawidhi Idara ya Ukuzaji wa Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mkoa wa Tanga Omari Ally Mohamed akieleza jambo wakati wa ziara hiyo