Idara ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere, wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya. Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la Uturuki yenye Namba TK 603, wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa Raia wa Sweden na Belgium.
Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.
Majina ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye mabano ni kama ifuatavyo;
2. SAMER HELMI KAMIT - SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI - IRAQ, PPT. NO. G 1111623
1 comment:
Hili swala si la kulichukulia kirahisi, especially ukizingatia kuwa tulishawahi kuumwa na nyoka before kwa terrorists kutumia nchi yetu km mahali pa kuishambulia Marekani.ie Embassy bombing. Na hii imetokea wakati ISI wameahidi kulipiza kisasi kwa America kuwapiga mabomu huko northern Iraq.
Tujiulize tangu lini Tanzania inapata wazamiaji kutoka Iraq, Syria etc?
Post a Comment