Wednesday, July 22, 2015

MSAADA WA USAFIRISHAJI WA VIFAA VYA KIJAMII KUTOKA WASHINGTON, SEATTLE MAREKANI KWENDA ZANZIBAR

Ndugu Zangu
Napenda kuchukua nafasi hii adhimu mbele yenu kuandika mada yangu tukufu kama ilivyotanjwa hapo juu.

Kwa niaba yangu binafsi, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla waliopo hapa Washington State na Nchini Marekani napenda kutumia nafasi ya kutoa maelezo ya vifaa vilivyopo hivi sasa katika Storage zetu kwa hatua kuvisafirisha kutoka Bandari ya Seattle hadi Zanzibar.

Vifaa hivi vimekusanywa na mimi kwa mashirikiano wafadhili mbali mbali waliojitolea kwa ajili ya kusaidia juhudi za maendeleo huko Zanzibar Tanzania ikiwemo Sefrioui Bassidy Foundation vifaa hivyo ni meza (tables) , computers , vigari vya kubebea wagonjwa wasiojiweza (wheel chairs) , vitabu (books) , na kadhalika.


Madhumuni makubwa ya kukusanya vifaa vyote ni mchango kusaidia juhudi za kuondoa kero mbali mbali zinazowakabili jamii yetu huko nchini kwetu katika huduma za afya na elimu kama ukosefu wa vitabu katika maktaba zenu, huduma za computer bado ni ngumu kupatikana ipasavyo katika shule mbali mbali pamoja na Hospitali nyingi kukosa huduma za vifaa kama wheels chairs na Walemavu kwa ujumla.

Napenda kutumia fura hii kama changamoto kuwaomba ndugu zangu Raia wema kutoka Nchini Marekani , Tanzania na Zanzibar kwa ujumla hususan waliopo nje kwa nia njema kuchangia hali na mali misaada ya kifedha kwa ajili ya Usafirishaji wa vifaa vyote viliopo sasa kutoka Seattle hadi Zanzibar mwezi July 2015.

Gharama za container lenye futi 40 ni dollars 6,500 bei hii imetokana na utafiti tuliofanya kupitia shirika la meli la Delma shipping line, Michango yote inakaribishwa kwa wote kwa kiwango cha aina yoyote na kutumwa katika account zifuatavyo

Jina : AMIN IBRAHIM ALLY
BANK OF AMERICA WA ACCOUNT NO 32000473
BANK OF CHASE WA ACCOUNT NO 622920028


Mchango unakaribishwa pia kwa njia cheque kwa jina hapo juu katika anuwani ifuatayo

1616 156th AVE NE APT 230 BELLEVUE WA 98007

7 comments:

  1. Mawazo mazuri ndugu yangu mzanzibar. Kwavile unatanguliza uzanzibar basi ni vizuri ukaomba misaada kutoka kwa wazanzibar na si Watanzania. Inafurahisha saana kuona wenzetu mnavyo ukana utanzania. Kwanini usiseme ndugu zangu watanzania? Tanzania ina mikoa 30 tu. Bara 25 na zanzibar 5. Ndugu yangu rekebisha kiswahili chenu hicho cha mimi mzanzibar lakini natoka Tanzania maeneo ya sharif shamba.....

    ReplyDelete
  2. unaposema wazanzibar na watanzania una maana ya nini?kwani sisi siwatanzania tu,

    ReplyDelete
  3. jamaiii eeeh eeeh,eeeh.mhusika mmemsikia kajinasibu kusema yeye mzanzibari?au mnaleno moyoni?na mtakuwa mnamjua si bure na choyo chenu cha rohoni.

    kaa mpime watu wanapeleka makontena dar na mikoa mingine na wazanzibari wanachangia au hamjawahi kuona?

    yeye kulipeleka huko Zanzibar imekuwa nongwa,mwaoo?

    aaah vibayeni hivyo kuweni wastaarabu huna cha kuchangia kaa kimya msilete midomo yenu merefu kama samaki wa chuchunge.

    kumbukeni Zanzibar ni nchi si mkoa wala si wilaya akisema hiyo Zanzibar si kitu cha ajabu.

    wazungu wanavyotusaidia mbona hawasemi sisi si waafrica kwa nini tuchangiye/au sisi si watanzania.

    dunia mapito,na hapa tupo ugenini hujui nani atakuja kukufaa leo au kesho unaye mdhaniya atakuja kukufa mungu anaweza kumgeuza nia na asikufae hata akiwa mwanao,na usiyemdhaniya anaweza kuja kukufaaa.

    tuwe na utu na ubinadamu tukiweza kuchangi tuchaniye tusipoweza tukae kimya kwani utapungukiwa na nini ukikaa kimya.mdomo mdomo mwingi mara nyingi hukuondolea thamani yako ya utu na heshma yako.

    mungu atusadiye tuwe na miyoyo ya kushikamana kidhati,kupendana,kuoneana huruma na kuwa kitu kimmoja na kudumisha undugu wetu wa kitanzania.

    hatuwezi kutengana tena tumeshachanganya damu na kukaliana so tusibaguane.

    Aliye na moyo wa kweli wa kutoa atatoa na asiye nao mungu amjaliye awe nao amen.binadamu kufaana leo kwako kesho kwa mwenzako.

    usife moyo amin.unania mzuri na njema mungu yupo pamoja na wewe utafanikiwa tu kulipeleka container na kuwasaida walio nyumbani. Ameen.

    kwa yeyote niliye mkwaza naomba samahani kwa sababu ulimi hauna mfupa.

    ReplyDelete
  4. Ndugu muhusika napenda kujibu suala lako kama ifuatavyo hapo chini
    Jawabu sahihi hapa kuomba msaada wa kuhakikisha vifaa vinaondoka katika kusaidia jamii ya nchi yetu ya Tanzania ikiwa Zanzibar au Tanzania bara kwa hiyo ikiwa nimekosea lugha kuambatanisha wazanzibar au Watanzania naomba kwa hilo sina nia kubagua eneo lolote katika Tanzania yetu kwa hiyo naomba wale wote waliokuwa na uwezo wa kutoa michango yao wanakaribishwa wakati wowote katika kutoa michango hiyo vifaa vyote vinakwenda kusaidia matatizo ya wananchi katika nchi yetu na bara la Africa kwa ujumla

    Naomba wote ambao wanataka kuwasiliana na mimi kama muhusika katika suala hili wanaweza kuniandikia katika email yangu
    aminallybts161@live.com
    206-372-1693
    Napenda kuwakilisha hoja yangu

    Amin ally

    ReplyDelete
  5. Samahani muhusika kama nimekosea lugha yangu katika masuala ya kuandika baina ya wazanzibar na watanzania napenda kuomba radhi ikiwa mkono wangu katika maandishi ya kuomba msaada huu umekwenda mbali zaidi nia kuomba msaada kwa watanzania wote kutoka pande mbili za muungano wa Tanzania ikiwa Zanzibar au Tanzania bara kwa hiyo tumia neno Mtanzania au watanzania kuondoa hizo hitilafu za maandishi au eneo la Nchi

    Naomba wahusika kuchukua ombi kwa Watanzania wote nakaribisha michango yenu

    Ahsante

    Amin

    ReplyDelete
  6. Amina Ally una busara za ajabu, nimefurahi sana jinsi ulivyotuelewesha kuhusiana na hili suala, na naamini kila mtu atakubaliana na maelezo yako (Mungu akubariki sana kwa roho yako njema). Ila huyo anonimous wa July 20, 2015 at 8:57 AM anaonekana kuwa na jazba kweli. Uandishi wake unanipa mashaka kama ni mtanzania au ana sili ya Mombasa.

    Asante Amina

    ReplyDelete
  7. hata na mimi uandishi wako unanipa mashaka kama ni mtanzania halisia au mkimbizi katika nchi yetu.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake