ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 13, 2015

ITV washushiwa Rungu na TCRA,Kisa Kusema Uongo Kwenye Maandano ya lowasa Juzi

EDWARD Lowassa ni kama ameanza kuipa majanga kituo cha Televisheni Cha ITV ndivyo naweza kusema baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kukitaka kituo hicho kuomba radhi mara mbili mfululizo kwenye taariifa zake za habari pamoja na kupewa onyo kali baada ya kukiuka sheria ya utangazaji nchini ya Mwaka 2005.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hukumu hiyo ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi (pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Muyangi amsema kamati hiyo imebaini kituo cha ITV kulikiuka sheria hiyo ya utangazaji nchini kwa kurusha taarifa ambayo ingeweza kuleta machafuko nchini.

Amedai katika kipindi cha Habari zilizotufikia mda huu kilichorushwa siku ya Jumatatu ya tarehe 10 mwezi huu majira ya saa 2.22 asubuhi ambapo katika kipindi hicho kilirusha taarifa kuhusu “Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati wa kumsindikiza Lowassa kwenda kuchukua fomu ya Urais.

Amesema katika kipindi hicho Mtangazaji wake alisikika akisema Jeshi hilo limezuia maandamano hayo baada ya kubaini yanauvunjifu wa amani huku Mtangazaji huyo akimnukuu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akidai ndipo amesema hivyo,Wakati taarifa hiyo ilikuwa ya upotoshaji kwani jeshi hilo alikuwa alijasema taarifa hizo..

Muyangi amesema baada ya ITV kurusha taarifa hiyo ya kwanza juu kuzuiliwa huko kwa maandamano, ndipo siku hiyo hiyo tena katika kipindi hicho cha Habari zilizotufikia mda huu majira ya saa tatu asubuhi kilirushwa taarifa inayosema Jeshi la Polisi limeruhushu maandamo ya Chadema kutoka Makao makuu wa Chama cha Wananchi CUF Buguruni Jijini Dar es Salaam kwenda Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC amedai katika taarifa hiyo ilisikika sauti ya Kamanda Kova juu ya kuruhusu maandamono hayo,tofauti na taarifa ya kwanza haikuweka uthibitisho wa Kamanda Kova.

Amesema Baada ya Mamlaka hiyo kubaini makosa hayo,Kamati hiyo iliwasiliana na Mkurugenzi wa Itv Be Mhavile na mkurugenzi wa Redio one Deogratus Rweyunga pamoja na Mhariri wa ITV Steven Chuwa.

Ili kutaka ufafanuzi ambapo wote kwa pamoja walikili kosa hilo huku wakisema Mtangazaji huyu alitoa taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii ambayo ilikuwa inakataza maandamano hayo ambapo alishindwa kuithibitisha kama taarifa hiyo kama ni ya kweli au la.

Aidha, Be Muyangi amesema baada ya Kamati hiyo kusikiliza pande zote,ndipo wakatoa hukumu kwa kupitia sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 ambayo inakataza kituo chohote cha Utangazaji kurusha taarifa zinatazoleta mchanganyiko katika jamii,

Ndipo wakatoa hukumu ya kuitaka ITV kuomba radhi mara mbili kwenye taarifa za habari ya asubuhi na jioni kwa


nzia hukumu hiyo ilipotolewa leo na kupewa onyo kali.

2 comments:

Anonymous said...

Oops ndo maana mswada wa habari ulipita wangu wangu
Ili mtukomeshe
Mmeula na chua tunajuwa sheria kuliko mnavyoijua mafisadi nyinyi wa CCM
Nawachulikiwa viongozi wa CCM Kama Hitler

Anonymous said...

Sheria lazima zifuatwe. Hali ya kisiasa ilivyo nchini ITV haikupaswa kutangaza zuio la maandamano ya CDM, jambo ambalo halikua na uthibitisho. kufanya hivyo ni kulichonganisha Jeshi la Polisi na wenye mapenzi na CDM. ITV ilionyesha ushabiki pasipostahiki.