ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 23, 2015

MISS TANZANIA USA: MAJAJI WAMPOKONYA USHINDI DOREEN PANGA NA KUMVIKA TAJI AEESHA KAMARA NJE YA UKUMBI

Aeesha Kamara sasa ndiye mshindi wa Miss Tanzania USA pageant
  Miss Africa 2014-15 akipata picha ya pamoja na Doreen Panga baada ya kuvikwa taji la Miss Tanzania USA 
Miss Africa 2014-15 akipata picha ya pamoja na Aeesha Kamara baada kuvikwa taji na maamuzi ya majaji ambao hawakukubaliana na mshindi aliyetangazwa kwanza.

Doreen Panga kutoka New York usiku wa Aug 22, 2015, alivuliwa taji la Miss Tanzania USA na majaji wa shindano hilo nje ya ukumbi taji alilolivaa kwa dakika 45 na kumvika Aeesha Kamara wa Maryland kwa madai kwamba Doreen Panga hakua chaguo lao.

Majaji hao Peter Walden, Elaine Roecklein, Tee Thompson, Bertini Huemegni, Tina Semiti Magembe, Mayor Mlima, Uche Ibezzue wakiongozwa na Michael Lewis McBride kwa pamoja walikataa kukubaliana na mshindi aliyetangazwa na kufanya kikao nje ya ukumbi wakati watu wakiondoka ondoka huku nao wakisikitishwa na maamuzi ya kutangazwa mshindi ambaye hawakumtarajia.

  Kama majaji wangekaa kimya basi masahabiki wa shindano hilo wangepelekea lawama kwa majaji.Jaji Dr. Secelela Malecela japo kwamba alipingana na Doreen Panga kutangazwa mshindi lakini hakukubaliana na majaji wenzake Doreen avuliwe taji na apewe Aeesha Kamara aliyekua chagua la majaji wengine, yeye alipendekeza kwa kua kosa lishafanyika waachane nalo wahakikishe mwakani halitokei tena. Wazo lake lilipingwa na majaji wenzake pale pale.

Shindano hilo lilianza vizuri kwa nyimbo za Taifa za Marekani na Tanzania zilizoongozwa na watoto Brian akiwa kwenye kinanda na dada yake Briana akiwa kwenye kipza sauti,

Baadae walitambulishwa ma miss wa kesho watoto wa DMV wenye umri wa miaka 9 na 12 na baada ya hapo waliingia malikia wenyewe huku wakisindikizwa na wimbo wa Diamond wa mdogo mdogo na baadae kujitambulisha kwa majaji.

Washiriki wa miss Tanzania USA walikua Rechel Mujaya kutoka Atlanta, Joyce Mkapa toka New York, Doreen Panga toka New York, Aeesha Kamara toka Maryland, Aziza Gama toka Maryland na Brenda Panga toka New York. Washiriki walianza shindano kwa kujielezea wakifuatia na shindano la vipaji na baadae kujibu maswali ya majaji.

Pia katika shindano hilo kulikua na burudani mbalimbali akiwemo Mr Tz ambaye aliitambulisha singo ya wimbo wake mpya uliotoka mwezi uliopita, Wasanii wengine walikua kutoka Ivory Coast na Jamaica.

Baada ya hapo ndipo kulitangazwa mshindi kuwa ni Doreen Panga ushindi ambao waliowengi hawakukubaliana nao wakiwemo majaji na mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Bi. Lady Kate ambao walisikika wakinong'ona huku wakiulizana imekuaje bila kupata majibu.

Wakati majaji wakiwa nje ya ukumbi wakitafakali imekuaje tumeacha shughuli zetu tumekuja hapa tunatoa maamuzi sahihi halafu mtu anatuzarau maamuzi yetu. Mashabiki walianza kuondoka baada ya shindano hilo kufikia ukingoni na wengine wakimtupia lawama wandaaji kwa kuvurunda shindano.

Majaji walipokua wakijadiliana wafanye nini walikuja na kuazimia kwa kauli moja  lazima wampe ukweli mwandaaji kwamba hawakufurahika na kilichotokea ndani ya ukumbi. Mwandaaji wa Miss Tanzania USA Ma Winny Casey aliitwa na majaji wakatoa dukuduku lao na mwandaaji akajitetea sio yeye kwamba mshindi amesema hataweza kushiriki mashindano hayo na ameamua kumpa taji mshindi wa pili ambaye alikua Aziza Gama, baada ya kusikia hayo majaji walimwita Doreen Panga na kumuuliza sababu yake ya kutaka kumvisha taji mshindi wa pili ni nini yeye akawajibu ni kutokana na kazi zangu ninazofanya hospitali sitaweza kupata muda wa ushiriki kwa hiyo badala yake nitampa taji mshindi wa pili.

Majaji walishindwa kuafikiana na Doreen na kuamua kupiga kura upya ndipo wote kwa pamoja  walimchagua Aeesha Kamara kwamba ndiye aliyestahiki kuvigwa taji na ndio aliyekua chaguo lao. Dr Secelela Malecela yeye alikataa kupiga kura hiyo.

Doreen Panga akavuliwa taji na kuvikwa Aeesha Kamara huku Doreen akionesha kutokubaliana na majaji lakini wao ndio waamuzi wa mwisho na kitendo walichokifanya ni kulinda heshima yao.

Sasa Miss Tanzania USA ni Aeesha Kamara, mshindi wa pili ni Aziza Gama na mshindi wa tatu ni Joyxe Mkapa.





4 comments:

Anonymous said...

Ya jana kaliiiiii kuhusu Miss Tanzania.

Anonymous said...

Ni upendeleo wa aina fulani ulioonekana na kwa ujumla hatutakuwa tayari kushiriki mashindano haya chini ya waandaaji hawa wa kuzingatia ukabila ndani ya US!!??

seif msabaha said...

Roreen was free heart young lady, she was happy with the second results

Anonymous said...

Mambo ya aibu saaaaaaaana ,upendeleo wa wazi rushwa nje nje, kila kitu kilikuwa ovyoooooooooooooo!Ovyo kabisa!

Acheni kupotezea watu muda wao .Shughuli ya wabongo intertainment za kiwest si utumbo huo?
Jamaa anaongea kifaransa anajijibu mwenyewe!

Ma Wnnny nakupenda ila sitothubutu kamwe kumushauri mwanangu ajiunge chini ya uongozi wako. Huu ni udhalilishaji wa kijinsia. Unabagua kwa majina mchana kweupeee!!!!