Saturday, August 15, 2015

MTABIRI: KIFO CHA MGOMBEA URAIS KIPO PALEPALE

Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya.
Na Gladness Mallya
MTABIRI maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya ameibuka na kusema kwamba utabiri aliowahi kuutoa kwamba kuna mgombea urais atafariki, bado upo palepale.
Akipiga stori na gazeti hili, Maalim Hassan alisema kuugua ghafla kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ni dalili tu za ukamilifu wa utabiri wake lakini suala la mgombea urais kudondoka na kufa akiwa jukwaani akifanya kampeni linakuja.
“Kuugua kwa Mbowe hakujatimiza utabiri kama ulivyosema ila hizo ni dalili tu lakini kuna mgombea atadondoka jukwaani akifanya kampeni na atakufa lakini haioneshi ni wa chama gani na hii ni kutokana tu na mwaka huu ulivyoanza kinyota,” alisema mtabiri huyo.
Mwaka huu mwanzoni mtabiri huyo alitoa utabiri uliyoonyesha kwamba kutakuwa na kifo cha mgombea urais pamoja na mambo mengine ikiwemo kuibuka kwa magonjwa ya kushangaza.

7 comments:

  1. Mwanga mkubwa wewe na CCM
    Jitabirie wewe utakufa lini
    CCM mmezoea kuamini uganga
    Ukawa ni ya mungu

    ReplyDelete
  2. CCM. Kwa ushirikina
    Nafikiri hata ikulu kuna idara ya vood (ushirikina )
    Dunia ya leo tunaendeshwa na sayansi na technology
    Na huyu mganga mwanga kutabiri ya uongo CCM na serikali walk hamchukulii sheria
    Kisa yupo CCM
    Kama mtabari anawangie mimi basi niliopo ughaubuni
    Mwanga mkubwa na tapeli fisadi

    ReplyDelete
  3. HUYU BWANA SIMTOFAUTISHI NA MZEE WA KIKOMBE. THIS IS CALLED PROBABILIY IN MATH.

    ReplyDelete
  4. Yeye akiumwa hujitibia
    Au huenda hospitali
    Tapeli hili kama merehem baba yake

    ReplyDelete
  5. Mbona hakumtabiria kifo babake? Tupeane sayansi ya utabiri wako

    ReplyDelete
  6. Naona jamaaa kajipa kazi ya Mungu sasa. Manake ndie ajuae saa za mwanaadamu.Hivi huyu si alitabiri kuwa katiba itapita kwa kishindo?? lakini naona mpaka leo imekwama na tunaisahau sasa.

    ReplyDelete
  7. Neno la MUNGU wa mbinguni aliye hai linasema Sitakufa bali nitaishi ili nisimulie matendo makuu ya Mungu. Hivyo hatafufa mtu mpaka shauri la bwana Mungu litimie kwa jina la Yesu! na Yesu alipokufa alienda kuzimu ili kuharibu kazi za muovu shetani mojawapo ikiwa ndiyo hiyo, na kwa mtaji huo imeandikwa njia yake huyo anayepanga vifo vya watu na iwe giza na utelezi malaika wa bwana akiwafuatia kwa jina la Yesu. Na imeandikwa pia waaibishwe wafedheheshwe wanaoifuata nafsi , warudishwe nyuma wafadhaishwe wanaozua mabaya. Uharibifu umpate kwa ghafla , na wavu aliouficha umnase mwenyewe, kwa uharibifu aanguke ndani yake. Na nafsi zetu wote tupendao mema tutamfurahia BWANA. Bwana Yesu asifiwe.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake