Sunday, August 16, 2015

PICHA: MAELFU YA WANANCHI WAJITOKEZA KWENYE MKUTANO WA UKAWA JIJINI MWANZA LEO

Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza ukiwa umefurika kwa wingi katika Barabara inayoelekea kwenye Uwanja wa Furahisha, kulikofanyika Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa Mgombea Urais na Makamu wake wa UKAWA kupitia CHADEMA na kutambulishwa kwa wananchi, Agosti 16, 2015. Picha na Othman Michuzi
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza, leo Agosti 16, 2015, wakati wa Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na kutambulishwa kwa wananchi, Agosti 16, 2015.


 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza, leo Agosti 16, 2015, wakati wa Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa Mgombea wao wa Urais na kutambulishwa kwa wananchi, Agosti 16, 2015. 
Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa. Mama Regina Lowassa akiwasalimia wakazi wa Jiji la Mwanza, leo Agosti 16, 2015, wakati wa Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na kutambulishwa kwa wananchi, Agosti 16, 2015.




























8 comments:

  1. Chaguwa Ukawa tarehe 25 October

    ReplyDelete
  2. Hivi mafuriko haya yana vitambulisho vya kupiga kura.
    kama jibu ni ndiyo mzee asubiri kuapishwa tu.
    wanabidi kuzidi kuamasisha tar 25/10/2015 kupiga kura

    ReplyDelete
  3. Hakuna Hakuna
    Lowassa chaguo letu

    ReplyDelete
  4. yale yale ya mwaka 1995. napita tu.

    ReplyDelete
  5. huyu mzee anaonekana mgonjwa sana

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake