Wednesday, September 30, 2015
CCM WALAANI WAFUASI WA UKAWA KUFANYA FUJO KWENYE OFISI ZAO TANGA
Chama cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kupiga mawe na kutupa chupa, baadhi zikiwa na mikojo, kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga jana, tarehe 28 Septemba 2015, kabla na baada ya mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tangamano, Tanga Mjini.
Kama ilivyo kawaida yetu miaka yote, CCM iliazimia kufanya kampeni za amani, zinazoheshimu sheria za nchi na utu wa wapinzani wetu. Hadi sasa, tumeweza kuwadhibiti wapenzi, washabiki na wanachama wa CCM wasifanye vitendo vya ufunjifu wa amani. Tukio la Tanga sio la kwanza.
Tarehe 27 Septemba 2015 viongozi wa UKAWA waliwapanga vijana, katika eneo la stendi ya Uyole, mkoani Mbeya ili wasimamishe msafara wa Mgombea wa Urais wa CCM na kumfanyia vurugu na kumpigia kelele ili wananchi wasimsikie vizuri.
Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi. Lakini viongozi wa CCM wa ngazi zote wamekuwa wanawahimiza wasifanye mambo haya kwasababu CCM hatuamini kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuomba ridhaa ya Watanzania kuliongoza taifa letu na pia, kwa kuwa sisi ndio tuliokabidhiwa na Watanzania nchi hii kuiongoza, tunafahamu dhamana yetu kubwa ya uongozi wa taifa na ulinzi wa amani ya taifa letu.
Tunawasihi wenzetu wa UKAWA kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kilichobaki, tufanye kampeni kwa amani ili tumalize uchaguzi kwa amani na taifa liendelee kuwa na amani baada ya uchaguzi. Wenzetu wa UKAWA wasitufikishe mahala ambapo washabiki wa CCM watashindwa kuvumilia kuona Chama chao na viongozi wao wanadhalilishwa. Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga. Hata hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi.
Chama chetu kina dhamana ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo hawana. Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa. Tunawapongeza wana-CCM kote nchini kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni.
Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi. Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia kwamba mkutano wa kampeni unaahirishwa kwasababu ya wingi wa watu.
Katika mikutano ya kampeni, ikiwemo ya CCM, na hata katika sherehe za kitaifa, baadhi ya watu huzidiwa nguvu na huhudumiwa na wahudumu wa huduma ya kwanza huku mikutano ikiendelea. Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wenzetu kutafuta kisingizio cha kutofanya mikutano ya kampeni. Mkutano wa kampeni ya UKAWA wa Geita pia waliuahirisha kwa kisingizio tofauti, kwamba jukwaa na vipaza sauti havikuandaliwa ingawa aliyetangaza kuahirisha alisimama jukwaani na akasikika na watu wote.
Mabadiliko wanayoyahubiri wenzetu yanaanza na kusema ukweli. Imefika mahali sasa wenzetu wa UKAWA wawaeleze ukweli Watanzania kuhusu mgombea wao kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano au kuhutubia kwa dakika 3 kuliko kuwahadaa kwa kutengeneza matukio na vioja ili kuficha mapungufu ya mgombea wao.
Tunarudia kuwataka viongozi wa UKAWA kuacha kupanga vurugu, kuharibu mali za CCM, na kutukana wana-CCM. Tunarudia kuwataka waache kauli zao za kuibiwa kura. Kauli hizo ni za kukata tamaa na kuwandaa watu kufanya fujo.
Tunadi sera zetu na wagombea wetu kwa amani ili tuwape Watanzania fursa ya kuchagua kwa amani ili taifa liendelee kuwa la amani, umoja, utulivu na mshikamano mara baada ya uchaguzi.Imetolewa na: January Makamba Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM 29.09.2015

Kipara mtoto mdogo
ReplyDeleteUna nini wewe
Hizi ninngonjera ambazo waTanzania na wapenda amani bado tunashindwa kuzielewa kuna fuko zinaanzishwa au kipangwa kabisa na Chama tawala lakini zinahesabiwa ni za kutoka upinzani! Tulioona sivyo inavyoandikwa. ! Ya mkutano.kuahirishwa tuliokuwepo tuliona hali halisia na ilikuwa maamuzi mazuri kutotokea yale ya Morogoro. Hivyo mwandishi umeeleza uliyodhani yanawafaa waTanzania na wasomaji lakini sio hivyo bora ungekuwepo tungeelewa. Swala la ushindi usiliwekee sana uzito.kwaninwawilinwapambanapo mmoja ataibuka na ni yeyote yule sasa unaposema tumeshinda wao wameshashindwa unadhani umeweka umathubuti!! Au ni yale ma h oli ya mkono ndio yanayotoa nguvu!!
ReplyDeleteSafii achana nawahuni
ReplyDeleteHata mkikataa vipi Ukawa mmethibitisha kuwa mnapenda vurugu. Mmempiga kwa chupa Polisi wa kike Dodoma. Mmempiga mawe Polisi Iringa. Mmevamia msafara wa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM huko Mbarali na mkafanya funyo zilizopelekea Polisi kuingilia kati. Hayo Tanga, Nape kaeleza. Huko Singida kiongozi mmoja wa chama chenu amempiga mateke mama mmoja kwenye mkuatno wenu na kumpasua mfupa - haya ni baadhi tu ya matukio mliofanya. Ni kielelezo gani kingine mnataka kitoelewe ili muweze kufahamu kwamba nyinyi siyo waungwana? Je kama mkiingia Ikulu (Mwenyezi Mungu pishilia mbali) na tabia kama hii Watanzania watasalimika?
ReplyDelete