Thursday, November 12, 2015

KOVA: TUNAMSHIKILIA MSHIRIKA WA LOWASSA


JESHI la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini, imekiri kumshikilia mshirika wa aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA); kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Edward Lowassa, Bashiri Awale, kwa uchunguzi zaidi kwa kile kilichodaiwa uraia wake una utata.
Akizungumza Dar es Salaama jana katika mkutano wake na waandishi wa habari Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova, alisema; "Ni kweli tunamshikilia na kumchunguza Awale kutokana na tuhuma zinazomkabili."
Alisema inaonekana kuwa mtuhumiwa huyo ni raia wa Kenya na hata hati yake ya kusafiria namba C000529 inaonesha ni ya Kenya inayoonesha alizaliwa Julai 11,1969 jijini Nairobi.


"Ni kweli Jeshi la Polisi linamshikilia Bashiri Awale Mwanaharakati wa CHADEMA, ambapo mtu huyu tulimkamata Novemba 9, 2015 kutokana na tuhuma zinazoambatana na utata wa masuala mazima ya uraia wake na jinsi ambavyo amekuwa akijihusisha na masuala ya kisiasa nchini Tanzania," alisema Kamanda Kova.

Alisema mbali na pasi hiyo ya kusafiria kuonesha ni raia na mzaliwa wa Kenya katika Jiji la Nairobi, lakini baada ya kukamatwa na kupekuliwa nyumbani kwake eneo la Mikocheni alikutwa na cheti cha kuzaliwa namba D063711 kwa jina la Bashiri Abdi Ally kilichoonesha amezaliwa Julai 11,1969 katika Hospitali ya Serikali mkoani Dodoma, nchii Tanzania.

Alisema kumbukumbu hizo zinazokinzana zimeleta utata, hivyo wanaendelea kumhoji kwani kwa na uraia wa nchi mbili ni kosa chini ya sheria za uhamiaji.
Alisema zipo tuhuma zinazonesha kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akijihusisha kikamilifu na siasa za Tanzania hususan katika kipindi cha uchaguzi uliomalizika, jambo ambalo ni kinyume na katiba mwaka ya Tanzania ya 1977.
Aliongeza kuwa Katiba ya Tanzania haimpi nafasi mgeni yeyote kuchagua,kushiriki katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais,wabunge na madiwani na inatoa haki kwa raia husika kushiriki kikamilifu uchaguzi huo.

Majira

10 comments:

  1. Jeshi la polisi linafanya kazi kwa muongozo wa CCM, kazi yake kubwa kukamata wapinzani badala ya kulinda amani na kukamata majambazi, wezi, wezi wa mali za umma na wapokeaji rushwa. Sasa kama wamemkuta anayo cheti cha kuzaliwa kutoka Dodoma Hospital wanamkamatia nini? Mimi mwenyewe mtanzania lakini sina cha cheti wala karatasi lolote kama ilivyo kwa watanzania wote waliozaliwa kabla ya 1971....hatukupewa vyeti tuliozaliwa wakati huo. Bashir Awale alifanya kazi miaka mingi Tanzania na amezaliwa Tanzania ila kwa sababu ana asili ya kisomali ndiyo serikali, CCM na polisi wake wanamnyanyasa......Mbona hawamhoji Aden Rage?? au kwa vile yupo CCM? Mbona hamuwahoji wahindi wanaoishi Tanzania kama kina Ketan Somaia, Jituson, Sethi wa Escrow na wengine wengi walio na uraia wa nchi zaidi ya nne (CANADA, UK, USA,HONG KONG, INDIA na TANZANIA?) Mbona hatuoni LAZARO NYALANDU akihojiwa wakati ana uraia wa USA? Acheni DOUBLE STANDARD. Acheni uonevu pia, Hatutafiki kwa jinsi hiyo mmeanza kuwashughulikia wale wote walio-msupport Edward Lowassa, pamoja na kumwibia kura hamjatosheka tu??????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si kweli waliozaliwa kabla ya1971 hawana vyeti vya kuzaliwa mimi changu ninacho. Na sheria ni msumeno, kama wewe ni mtanzania nenda nje ushiriki ktk chaguzi halafu uone nini kitakachokukutokea. Shule nzuri jamani nenda soma elimu ya watu wazima pengeni utajifunza usiyoyajua

      Delete
    2. Mdau acha vyombo vya usalama vifanye kazi yake,shida kubwa ya watanzania ni ku politicize kila jambo.kuna mambo mengine hayahitaji siasa."You cannot claim to know the Ocean by sealing on it".

      Delete
  2. Siku zote tunasisitiza ya kwamba Tanzania na watanzania kwanza, na si kwa nia ya Kum'bagua mtu wa taifa jengine bali ni ya kudumisha na kujenga uzalendo wa kweli la sivyo ipo siku tutajikuta watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe. Leo hii kiongozi alietarajiwa kuwa muhimili mkuu wa nchi yetu anashirikiana na matapeli kuvunja sheria za nchi. Mueshimiwa lowasa amethibitisha tena na tena kuwa sio mtu anaejali na kuweka mbele maslahi ya Taifa tofauti na kauli zake . Kipimo cha ubora wa kiongozi wowote haupimwi na kauli zake bali ni vitendo. Fikiria kwamba kitendo hiki kilichofanywa na Lowasa kama kingelifanywa na magufuli ingekuwaje kwa upande wa upizani pengine wangetaka serikali zima ya magufuli ijiuzulu. Kwa kitendo cha timu Lowasa kufanya kazi na raia wa kigeni mwenye utata wa utambulisho wake pengine ikiwezekana hata kuwa moja ya viongozi wa kikundi cha kikigaidi cha Alshabab na anae tambulika kwa upande wa upizani kama mwanaharakati wao wa kumsaidia kuingia ikulu mueshimiwa lowasa kwa kweli ni usaliti uliokisiri wa hali ya juu katika usalama wa Taifa. Tuna imani watu wa aina hiyo wapo wengi tu Tanzania na tuanaiomba serikali iliopo madarakani kutilia mkazo katika kuwatambua. Watanzania wengi licha ya kuwa CCM ina matatizo lakini tutaendelea kuwa na mashaka jinsi ndugu zetu wa mikoa ya Arusha, Moshi na maeneo ya karibu ya mikoa inayowazunguka jinsi gani wanavyokadhania katika kuutukuza ukanda kwa nguvu zao zote kwa kisingizio cha part Strong hold. Na hasa baada ya huu uchaguzi uiopita utabaka na ukanda umetumika zaidi katika kukichagua chama na wagombea wao hilo halina shaka. kwa waafrica hakuna kitu part strong hold isipokuwa kuna part ethnic strong hold huo ndio ukweli. Kwa kuwa chama fulani kina viongozi kutoka katika matabaka yetu tutawasapoti kuwaweka madarakani hata kama ikiwa hawana uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kazi ilimradi tu ni watu wa jamii yetu. Siasa za kikanda zimekuwa zikiinyemelea Tanzania kwa muda mrefu shukrani kwa chama cha mapinduzi licha ya mapungufu yake mengine kimetuungoza katika kuepukana na kumuweka kiongozi madarakani kwa kutumia gear ya ukanda ila kuna ushahidi wa kutosha kabisa ya kwamba Chadema ni chama chenye mifumo ya kikanda ikiwa mtu atabisha na kuchukizwa na kauli hii lakini ukweli lazima utabakia pale pale. Ila licha ya kuwa uchaguzi umekwisha na CCM kufanikiwa kushinda uchaguzi bado watanzania tunahitaji chama sahihi m'badala wa CCM kitakacho waunganisha watanzania wote bila ya kuangalia anatoka wapi kama ilivyokuwa kwa CCM.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna utata mwingi kuhusu watanzania wengi wenye uraia zaidi ya moja na bado wapo serikalini lakini kwa vile wapo CCM hakuna wanachofanywa.

      Delete
    2. Ukiachia utata wa uraia wa huyu mamluki,kuna issue ya kuzaliwa siku moja katika nchi mbili tofauti.

      Delete
  3. Hebu watu tuache sisa kwenye mambo ya msingi na haswa haswa hili linalohusu uraia wa watu.Hapa tuache vyombo vya usama vifanye kazi yake bila kuingiliwa na mtu,maana tatakuwa tunawatisha kwa kusema watu wa mlengo fulani ndo wahanga wakati si kweli,hebu rudisheni kumbukumbu zenu nyma kuna watu waliokuwa na nyadhifa katika chama na serekali lakini ilipo bainika pasi na shaka kuwa wao sio raia wa tanzania walifukuzwa na kutakiwa kuomba vibali na baadae urai wa Tanzania mfano Generali Ulimwengu, Mwenyeki wa CCM Bukoba (aliyekuwa)hawa ni mifano tu.Hivi sasa kumekuwa na tabia kila mtu kutaka kuingilia maswala ya usalama kwa kigezo cha kuonewa kwa kuwa wao ni chama fulani,mtu akiguswa tu utasikia anaonewa kwa kuwa yeye ni mfuasi wa chama cha upinzani,kauli hizi hazifai kabisa na zinapaswa kupingwa na kukemewa waziwazi na wapenda amani, ,kwani hao hao mambo yanapoharibika wanakuja na maneno kuwa aliyopo madaraka ameshindwa kulinda wananchi.

    ReplyDelete
  4. Vip na huyo sijui Kinana. Kwanza na waweke huwo Uraia wa nchi mbili watu wako nje kutafuta maisha tu. Ndugu familia yote iko bongo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Waswahili wanasema,"Huwezi kujisafisha kwa kutumia tope " or " two wrong do not make one right ".Huyu bwana amekamatwa kwa kuvunja sheria ya nchi,na ahukumiwe kwa hilo.Kwakusema kuna akina X & Z nao sio raia haimuondoi kwenye kosa hilo.
      Acheni sheria ichukue mkondo wake..

      Delete
  5. It makes sense kumshikilia huyo Msomali mwenye Pasipoti ya Kenya. Watanzania tusisahau kuwa Kenya walishambuliwa na Wakenya wenye asili ya somali i.e. AL SHABAB terrorists. Tunayo haki na mamlaka kama nchi kuwapeleleza watu kama huyu jamaa. Ajabu ni kwamba bwana Lowassa hakuwa makini kuona ni nani wako kwenye kampeni yake, kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa nchi. Serikali isimwachilie huyu msomali mpaka Lowassa ajieleze Mahakamani kuhusu uhusiano wao, la sivyo awekwe na kuoza kizimbani.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake