Tuesday, November 10, 2015

Mahojiano na Liberatus Mwang'ombe katika kipindi cha JUKWAA LANGU

Liberatus Mwang'ombe katika moja ya mikutano yake jimboni Mbarali
Katika kipindi cha JUKWAA LANGU wiki hii tulipata fursa kuongea na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Mbarali kupitia CHADEMA Liberatus Mwang'ombe ambaye ameeleza mengi kuhusu uchaguzi ulivyokuwa, aliyojifunza, analotaka kufanya kuhusu matokeo na hata kwa wana-diaspora wengine wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali Tanzania

1 comment:

  1. Shukrani sana brother Bandio pamoja na brother Luke kwa program nzuri tu na kwa kweli binafsi hupenda kusikiliza zaidi na kuelewa kinachozungumzwa na nna promise kuja kuchangia something siku zijazo licha ya kuwa na tight schedule. Ila hapa nina ya kuchangia juu ya nilichokisikiliza na hasa kuhusu program nzima na balancing ya utoaji wa maoni.
    (1) kuhusiana na brother Libe na madai ya kuzulumiwa kura zake na madai mengine anayolalamikia. Kwangu mimi naona tumesikia one side story na waswahili siku zote wanasema msema pweke siku zote huwa mkweli je kuna jitihada zozote zilifanywa au zinafanywa kumpata mtu aliemshinda brother libe nae akatoa maoni yake.
    (2)kuhusu madai ya brother libe ya kwamba msafara wake kushambuliwa tena kwa risasi za moto. Katika hili vile vile linatia shaka sana hasa kutokana na matendo mengi feki ya vurugu yaliyokuwa yakifanywa na watu wa upizani wakati wa uchaguzi ili vionekane kuwa vilikuwa vikifanywa na chama tawala au wagombea wa chama tawala. Kuna hata baadhi ya wagombea wa upinzani kujaribu kujiteka nyara wenyewe ili kutafuta attention . Shukrani kwa serikali kuanzisha sheria ya mitandao kwani tumeona kuna watu ambao kesi zinaendelea kwa kutoa taarifa feki kwa umma wakati wa uchaguzi kwamba watu walishaanza kuuana katika maeneo mbali mbali na kukamatwa kwa boksi ya kura mbazo habari zote zilikuja kuthibitika kuwa feki.
    (3) jukwaa langu kama jina la kipindi ila jitihada za makusudi zifanyike ili kipindi kisionekane kama jukwaa la chadema na upizani peke yake. Ni wazo zuri kabisa tunaweza kusema labda kutojitokeza kwa wachangiaji wa chama tawala ndio kunatoa twaswira ya kuwa hichi kipindi ni kwa ajili ya upinzani hasa chadema ila kwa mtayarishaji wa kipindi mahiri mwenye nia ya kuiweka program yake ionekane iko balance na ivutie watu wa pande zote na hakika anajua nini cha kufanya.
    (4) Sikuwepo kwenye ground kama alivyokuwa brother Libe lakini naamini ameshindwa kihalali kabisa na kilochomfanya mwanadiaspora kushindwa ni kitendo cha kukataa kwa wapinzani kumsimamisha mgombea mmoja wa upizani that's all. Ikiwa mshindi kapata kura 45000 na Libe kapata kura 36000 na mageuzi kapata 20,000 sasa utaona hujuma hapo haikufanywa na CCM bali imefanywa na wanabaliko wenyewe. Na suala la kuilaumu tume baada ya kushindwa uchaguzi ni suala ambalo halina mshiko wowote wa maana sawa sawa na kwenda kumuadhibu mtoto wa kike baada ya kubeba ujazito usio halali ni kumuonea tu kwani jitihada zilikuwa zifanywe mapema na wazazi kuepusha yaliyomkuta. Na kuhusu tume, kila uchaguzi unapokwisha ni mwanzo wa uchaguzi mwingine kwa hivyo upinzani walikuwa na muda wa karibu miaka mitano kurekebisha mambo ikiwezekana kama tatizo ni tume basi walikuwa na uwezo hata ya kugomea uchaguzi mpaka wapate tume wanayoiafiki kwa kukaa kwao kimya na kuendelea na uchaguzi inamaana wapinzani waliridhika na tume. Na kuhusu kukataa na kupinga matokeo ya uchaguzi kwa visingizio mbali mbali kwa chadema na wagombea wake waliopoteza nafasi mbali mbali inaonekana ni mkakati maalum wa chama na wamekubaliana iwe hivyo kwa sababu haiwezekani wagombea wao wote walioshindwa wawe wameonewa lakini walioshinda mambo safi na tume nzuri. kama wanadiaspora nafikiri bila ya ushabiki lazima tupime na tuchoambiwa kwani tusijifanye tunajua sana na kuwaona wale kule nyumbani ni wapumbavu wasiojua kitu tutakuwa tunafanya makosa.
    .
    Pls the other two comments come by mistake release this one only.

    ReplyDelete