
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza
akipokea mashuka 150 kutoka kwa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) Mkoani Tanga, Ally Mwakababu kwa ajili ya vituo vitatu vya
Afya ambavyo ni Maramba, Mkinga na Lanzoni vilivyopo wilayani Mkinga mkoani Tanga. Picha na Oscar Assenga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza akiwa kwenye
picha ya pamoja na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF)
mkoani Tanga ofisini kwake mara baada ya kupokea mashuka 150 kwa ajili
ya vituo vitatu vya Afya,Maramba,Mkinga na Lanzoni vilivyopo wilayani
Mkinga mkoani hapa kulia ni Meneja wa NHIF mkoa wa Tanga,Ally
Mwakababu na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Salum Chima na
anayefuatia ni Afisa Matekelezo wa (NHIF) Miraji Msile.
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MKUU WA Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) mkoani hapa kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa
wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF)ili kuweza kuongeza
wigo mpana wa wanachama ambao wataweza kunufaika na huduma zao
Alitoa wito huo jana wakati akipokea mashuka 150 yaliyotolewa na mfuko
huo vyenye thamani ya shilingi milioni tatu yaliyotolewa na Mfuko huo
kwa ajili ya vituo vitatu vya afya vya Mkinga, Maramba na Lanzoni
vilivyopo wilayani Mkinga ambavyo zilikuwa zikikabiliwa na changamoto
ya uhaba wa mashuka.
Alisema kuwa endapo elimu itatolewa ya kutosha kwa wananchi wanaoishi
maeneo mbalimbali mkoani hapa hasa wale wa vijijini itasaidia kuongeza
idadi kubwa ya jamii inayoweza kunufaika na mfuko huo kwa ajili ya
kupata matibabu.
“Nisema kuwa pamoja na kazi kubwa mnayoifanya niwatake mhakikishe
mnaendelea kutoa huduma nzuri kwa wanachama wenu ikiwemo kuhakikisha
huduma za dawa hazikosekaniki kwenye vituo vya afya na zahanati ili
kuondoa usumbufu kwa wananchi
“Alisema RC Mahiza.
Hata hivyo alisema kuwa msaada huo umefika wakati muafaka ambao
wagonjwa na wananchi wanaokwenda kupata huduma kwenye vituo vya afya
wanakumbana na changamoto ya uhaba wa mashuka hivyo itasaidia
kupunguza makali ya kutokupatikana mashuka kwenye maeneo hayo.
“Mimi binafsi ni mdau na balozi mzuri wa mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) na nina vijana wangu sitini ambao watajiunga na mfuko huo
kwa lengo la kuhakikisha wanapata matibabu wakati wanapougua kwa
sababu maradhi yanatokea wakati wowote “Alisema RC Mahiza.
Kwa upande wake,Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani
Tanga(NHIF) Ally Mwakababu alimueleza Mkuu huyo wa mkoa kuwa dhamira
yao kubwa ni kuhakikisha wanasaidia huduma za afya kwenye maeneo
yalikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mashuka.
“Mkuu wa mkoa sisi tumekuwa mstari wa mbele kuweza kusaidia harakati
za kukabiliana na changamoto zinazopatikana kwa wananchi ambao
wamejiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kuhakikisha wanapata
matibabu na dawa kwa wakati muafaka bila kuwepo vikwanzo vya aina
yoyote ile “Alisema Mwakababu.
Aliongeza kuwa mikakati yao ni kuongeza ufanisi mkubwa katika
kuwahudumia wananchi waliojiunga na mfuko huo ili waweze kupata huduma
za uhakika wakati wanapokuwa kwenye vituo vya afya ili kuepukana na
usumbufu usiowa wa lazima
Mahiza mwatumu
ReplyDeleteOops
Cv ya uongo eti mwezi mmoja summer school ana diploma ya university of Oslo