
Mbeya. Raia wanne Wachina wanashikiliwa Kituo cha Polisi Kyela kwa tuhuma za kukutwa na pembe 11 za faru zinazodaiwa kutokea Msumbiji zikiwa na thamani isiyopungua Sh800 milioni.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Thea Ntara amesema leo kuwa raia hao wamekamatwa baada ya kutiliwa shaka na maofisa wa Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato (TRA) katika Kituo cha Kasumulu kilichoko mpakani mwa Malawi.
Amesema maofisa hao walilitilia shaka gari lao aina ya Prado na kuamua kulikagua ndipo walipogundua kuwamo kwa pembe za faru, na kuchukua hatua ya kuwaita polisi.
Ntara amesema pasipoti za Wachina hao zilionyesha walitoka Msumbiji kupitia Malawi.
Wakati ukaguzi ukiendelea, Wachina watatu walitoroka kutoka Kasumulu lakini walikamatwa tena mjini Kyela wakiwa kwenye teksi waliokodi iwapeleke Tukuyu, wilayani Rungwe.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi alipoulizwa juu ya tukio hilo alithibitisha akiwa wilayani Kyela na kwamba angetoa taarifa kamili baada ya kurudi Mbeya
Hata hivyo RPC Msangi amesema upelelezi bado unaendelea.
Hawa Wachina hawako current na news.Hawajui alie washika na minofu ya samaki sasa hivi ndio kila kitu.
ReplyDeleteWale mpaka wasome kwenye magazeti yao ya Chinese. Vinginevyo, wa kiume wataendelea kuingia vyoo vya kike na wa kike vya kiume!
Delete