Monday, November 9, 2015

WANACHAMA WA CHADEMA MKOANI MBEYA WALALAMIKIA UTEUZI WABUNGE VITI MAALUMU

Uteuzi wa wabunge wa viti maalumu kupitia Chadema umezua taharuki mkoani hapa na Kanda ya Nyanda za Juu kwa ujumla baada ya wanachama na viongozi wa chama hicho kuanza kulalamikia wakidai umetumika upendeleo.

Walalamikaji wanasema wanachama wa kike ambao walikuwa mstari wa mbele kukisaidia chama ‘wametemwa’ na kuteuliwa wanawake ambao kimsingi hawakuonyesha ushiriki kikamilifu katika chama na wa wananchi wa eneo husika.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya wagombea Ubunge kupitia Chadema na Ukawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jacob Kalua alisema kuna ubabaishaji na upendeleo usiokuwa na tija katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu uliofanyika ndani ya Chadema kwa vile walioteuliwa wengine hawajawahi kuonekana majimboni lakini wanashangaaa kuona wamepewa nafasi hiyo.
“Hapa simung’unyi maneno kabisa. Kwa mfano aliyeteuliwa mkoani Ruvuma, hata viongozimkoa huo hawamjui. Kutoka Iringa wameteuliwa watatu, lakini mmoja amejiunga Chadema hivi karibuni na jina lake linateuliwa. Hapa Mbeya ameteuliwa mmoja, lakini ushiriki wake kwenye chama unazidiwa na wanawake wengine walioomba nafasi hiyo waliopo hapa na huko mkoani Songwe ambako kuna majimbo matatu ya Chadema hajateuliwa mwanamke hata mmoja,’’ je hii ni halali?, alihoji.
Naye Katibu wa Chadema, Wilaya ya Mbarali Nicolaus Lyaumi alisema anashangazwa kuona majina ya wabunge walioteuliwa siyo wale waliotarajiwa na wanachama wengi mkoani Mbeya.
“Unajua lengo la wabunge hawa ni kusaidia ujenzi wa chama mkoa na wilaya husika , lakini sasa kwa uteuzi huu tunaamini kabisa bado kuna sintofahamu iliyo mbele yetu kwani watu waliomba wamepigwa chini,” alisema.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la ‘China’ alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema hawezi kuzungumzia chochote akisema hajapata orodha kutoka kwa viongozi wake na kwamba majina yaliyotangazwa hayaamini.
Alisema ‘binafsi kama mkoa bado hatujaletewa rasmi majina ya wateule. Hivyo tukiletewa tutakaa na viongozi wenzangu mkoa tutayachambua na ndipo nitakuwa na la kusema itakapobidi’.

CHANZO:  MWANANCHI

3 comments:

  1. Kazi kwenu Chadema, sasa mnaoneana na mnaibiana wenye kwa wenyewe? Mlisema CCM inawonea, inawaibia..blaah blaah blaah. Tuliwaambia Chadema is full of greedy people, wenye tamaa ya uongozi, na lengo lao siyo kuwakwamua wananchi. Ni kwa maslahi ya wachache tuu. Mnasema mmoja wa wabunge aliyepewa nafasi kajiunga na chadema hivi karibuni? Ha..ha..ha..ha, leo mmesahau kwamba Lowasa alijiunga na Chadema na siku hiyo hiyo mkamchagua awe mgombea wenu wa Urais? Sidhani kama Chadema itaweza kupata ushindi wa kwenda Ikulu hata hapo 2020.

    ReplyDelete
  2. Chadema grow up. Stop being a cry baby. Kila saa kuonewa. Why you all the time? Suck it up and get to business. Maybe if you spend your time in strategizing rather than complaining too much you will succeed.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza Chadema is full of greedy people ? CCM je ? Umelogwa

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake