VIJIMAMBO

Tuesday, December 15, 2015

WALIOUKATAA UWAZIRI WA MAGUFULI WAFUNGUKA SABABU



Baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotajwa kuwa waliukataa uteuzi wa rais John Magufuli kuwa mawaziri katika serikali ya awamu ya tano wameeleza sababu za kuchukua uamuzi huo.
Mmoja kati ya wabunge hao ambaye hakutaka jina lake litajwe aliamua kuelezea. Aidai kuwa yeye ni mmoja kati ya wabunge ambao walipata nafasi ya kuteuliwa na rais lakini alihofia majukumu mazito na kasi ya rais Magufuli hivyo akaamua kujiweka kando.

“Niliarifiwa juu ya uteuzi lakini baada ya kupima nikaona hapana siwezi kazi ya uwaziri, bora nibaki na ubunge wangu,” Mbunge huyo alimwambia mwandishi wa gazeti la Mtanzania.

“Kasi ya Rais Dk. John Magufuli ni nzito na kwangu ni ngumu na nilifikiri niko mimi peke yangu kumbe baada ya taarifa hizi nasikia na wenzangu wawili nao walikataa uteuzi,”aliongeza.

Hadi sasa wizara nne za serikali ya awamu ya tano hazijapata mawaziri. Wizara hizo ni wizara Fedha, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Miundombino, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
at 4:24:00 PM
Share

4 comments:

  1. AnonymousDecember 15, 2015 at 6:51 PM

    Serikali haina hela.Pesa zote zimetafunwa kwenye safari za JK na kampeni. Unafikiri nani anapenda kufanya kazi huku wizara hazina hela.

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
  2. AnonymousDecember 16, 2015 at 4:10 AM

    Kama hili usemalo ni ukweli, basi wataje hao walioukataa uwaziri ili wananchi tuwajue, otherwise they should just SHUT-UP! They are SELFISH and UNPATRIOTIC. Sielewi kwa nini walichaguliwa kuwa Wabunge? Wanakataaje kulitumikia Taifa lao? Ni Wapumbavu hao wote, and I mean what I say.

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
  3. AnonymousDecember 16, 2015 at 7:56 AM

    Hakuna aliyekataa. Waongo tu. Hata Mimi nilikataa; in my dreams!!!!

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
  4. AnonymousDecember 21, 2015 at 12:29 PM

    mimi nimependezewa na maamuzi ya watu hao kukataa uwaziri. wala si kweli kwamba wamekosa uzalendo bali they are honest. kazi waliyoiomba na wakahisi wanaiweza ni ubunge. ila nawasikitikia wale wanaotaka na kuuukubali uwaziri kumbe hawana moyo wala uwezo wa kuutumikia. shame on them! ni vyema kupata mawaziri ambao kweli wana moyo na uwezo wa kuzifanya kazi za uwaziri na si kuwa mzigo tu na majina tu kwamba tuna mawaziri kumbe ni mabomu majipu na mizigo. hongera magufuli endelea na kasi hiyo hiyo yule ambaye haiwezi ni vyema aseme tu ili wanaoweza waendelee.

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
Add comment
Load more...

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake

‹
›
Home
View web version
Powered by Blogger.