Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mchezaji wa kikapu wa kulipwa nchini Marekani, Mtanzania Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa kuanzisha na kukuza michezo pamoja na vituo vya Michezo hapa Nchini.
Mchezaji wa kikapu wa kulipwa nchini Marekani, Mtanzania Hashim Thabeet akisaini moja ya mpira mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Zawadi ya Mpira kutoka kwa Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu nchini Marekani Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu nchini Marekani Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini. (PIcha na OMR)
BOFYA HAPA KUJUA YUPO WAPI NA ANAFANYA NINI http://www.ridiculousupside.com/2015/3/10/8181743/will-hasheem-thabeet-be-given-another-opportunity-at-nba-level




Hivi kumbe Hasheem bado anacheza Mpira huko njeee?!?! Safi sanaaa! Anachezea team gani? Hasheem Nakuomba uendelee kupambani angalia ya dunia hii yasikuingilie Kati kijana!!!
ReplyDeleteNdugu yangu huyo Jamaa ni masifa tu,he doesn't have a team in NBA for now.
DeleteBy the way his career in NBA is over.
Anacheza wapi, hata hajulikani anachezea ligi gani, amepoteza mwelekeo kabisa. No 2. Anajulikana kama bonge la disappointed in NBA history. Kila team inamkataa sababu ni mvivu. Sijui huko TZ anaenda kumchuza nani
ReplyDeleteHuyu jamaa si niliskia hachezi tena NBA?alipigwa chini mhh haya wee
ReplyDeleteAcha ubishoo umeona Samantha kapewa kiwanja basi na wewe wafunga safari, ulikuwa unatembelea ikilu kama kwa mjomba ako sasa inakusaidia nini kuwa na tel ya JK na kutambaaa ! Unabaki kulipwa hela ya kula mazoezini hivi inachelewesha timu gani vile
ReplyDeleteJamani Mbona wakali hivyo kwani mnamdai Hutu jamaa.. Au kunamtu anamlipia bills humu. Basi mwacheni Kama amefulia in yeye, Hana time , bishoo hayatuhusu kunawatu wanaweza kumtumia Kuwa mshawishi tusiwe wepesi kujaji watunwengine tujitazame wenyewe kabla ya kujaji wengine. Samahani kwanilio wakwaza
ReplyDelete