Saturday, January 18, 2014

SHEREHE YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI NEW YORK


 Jumuiya ya Watanzania wa New York (ikijumuisha New Jersey, Connecticut na Pennsylvania) itafanya sherehe ya kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Jumapili tarehe 19 Januari 2014  Brooklyn New York. Kuanzia saa 11 jioni hadi saa 6 usiku.

 Anwani ya mahala sherehe itakapofanyika ni 
3386 Atlantic Avenue, Brooklyn, NY 
 11208

Kutakuwa na chakula na baada ya chakula na vinywaji pia kutakuwa na Talent show za watoto kuimba, Fashion show na Music kutoka kwa Dj Bilal. Rusha roho, Bongo flavor na Ndomboro kama kawaida. 
kati ya Essex na Shepherd. Watanzania na rafiki wa Watanzania wote mnakaribishwa. Kiingilio kitakuwa dola 15 kwa wakubwa na dola 10 kwa watoto. Vituo vya karibu vya treni J ni Norwood na Cleveland. Kumbuka Jumatatu ya tarehe 20 Januari 2014 ni Sikukuu ya Martin Luther King ambayo ni public holiday New York hivyo ni kusherehekea toka Jumapili hadi Jumatatu. Mungu ibariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Zanzibar. Kwa taarifa zaidi Wasiliana nasi kupitia:
 Email: info@nytanzaniancommunity.org
Wote mnakaribishwa.
New York Tanzanian Communityc/o Tanzania Mission to the   Tel: 201-252-7220
Website:
  https://www.facebook.com/pages/New-York-Tanzanian-Community-Inc/166418816757062

Huu ndiyo ukumbi wa sherehe hizo patakuwa hapatoshi miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzniar Oyeeeee

21 comments:

  1. Safi sana Tanzanian New York Community kwa kukumbuka sherehe hii. Je kwa sisi tunaotumia treni tutafika Vipi huko?

    ReplyDelete
  2. Chukua treni j hadi Cleveland au Norwood.

    ReplyDelete
  3. Katibu na Kamati ya sherehe ni safi sana. Big up!

    ReplyDelete
  4. Wana New York fungueni Madrassa ili watoto wenu wamjue Mungu wao. Msiendekuze sherehe tu. Mnao Ma-Ustadh hapo

    ReplyDelete
  5. New York watoto wanahitaji Madrassa ili wamjue Allah. Mtaulizwa nyinyi mnaendekeza Sherehe tu eti Mapindizi

    ReplyDelete
  6. Jamani Mapinduzi hayo Mkumbukeni Allah.hata Madrassa hamna hapo aibu nyinyi na Shetehe tu.

    ReplyDelete
  7. Napongeza kwa kufanya hii party ni kitu chema...
    Ila Bora msingepiga picha mkaweka...sehemu gani hiyo??Kabisa mlikosa sehemu inayofanana naku party?Mnaweka picha mbaya ya New York...Nani ana run hii kitu ? Ni ki gezo gani kimetumika bei cheee maana hapo ni sehemu ya dola mia mbili mia tatu....Badilisheni pahala bana au hii ni hujuma kwa wazanzibar!!?mbona uhuru tanganyika milifanya pahala pazuri..?

    ReplyDelete
  8. WADAU INGIENI KWENYE ISLAMIC FINDER WEKA ZIP CODE YAKO UTAONA MDRASA MENGI KARIBU NA KWAKO KAMA MTOTO WAKO HUMPELEKI MADRASA NI WEWE NA MUNGU WAKO USIWASINGIZIE WATU NAVIJI SHEREHE ZAO

    ReplyDelete
  9. New York TZ community hatutaki udini. Sisi ni Watz na kila Mtu na dini yake.

    ReplyDelete
  10. Na makanisa vile vile yafunguliwe. Wacheni fitna!

    ReplyDelete
  11. Tafadhalini msituletee udini hapa. Chama chetu hakifungamani na upande wowote.Uwe mkristo,mwislamu,,mpagani,bohora,baniani wote twende kazini. Mdau usilete mipaka kwenye chama chetu. Na FYI kamati ni hiyo hiyo iliochagua sehemu ya Uhuru na Mapinduzi.

    ReplyDelete

  12. New York Tanznain Communiy ni jumuia ya kwanza hapa United States,Canada na Mexico inao kutanisha watu kutoka sehemu mabali za tanzania na marekani bila kuanagalia cheo cha mtu, kabila lake, rangi yake, umri na dini yake. Chama- NYTC- hiki ndicho cha kwanza kinachojitemea kwa fedha bila kuobama watu wachange kabla ya sherehe. Vile vile,chama hiki kina mpango wa kujiunga na Izone ya new York kuendeleza masomo ya wanafunzi kwa kutuimia internet-matandao -WiFi
    kwa wale wanatafuta madarasa-wakati wao umepita

    Futaia link hii kwa maelezo zaidi
    http://schools.nyc.gov/community/innovation/izone/default.htm

    ReplyDelete


  13. Thanks Anicetus.....

    Thats whatup!!!
    We need more stuff more than sherehe.

    ReplyDelete
  14. kazi ipo kweli kuna watu wanataka taka makanisa yafunguliwe kwani hayapo na hizo sunday school hamna na hapa katika nchi hii si ndo yenyewe kwa dini hiyo so watu wakishauriana na wenzao wa dini inginewe mnaleta zenu mnataka wenzenu bado walala kama zamani halali mtu

    pelekeni watoto wenu madrasa nyinyi hata mkituambia zipp code za islamic finder tuweke tutafute madrasa usidhani hatujui tunajua ile mlio wengi ndo hivyo tena starehe kwenda mbele watoto kule kunawashindwa mnajidai kuwalea kiz ungu matokeo yake wanaharibikiwa na hiyo mitandao yenu

    pelekeni madrasa watoto wenu uhuru mapinduzi hayatakusaidiyeni kitu

    na anaye taka kufungua kanisa aende makanisa yapo mengi marekani au hajui kizungu tumfunguliye ya kiswahili na hayo pia yapo mengi

    kazi kweli ipo kwa ushindani wenu haya jiserekubeni

    ReplyDelete
  15. siku hizi balaa imekuwa watu kuambizana na kukatazana inakuwa ushindwani sijui chama hakifungamani na dini yeyote ile sijui nini na nini nani kakwambia hayo tunaambiwa serikali haina dini ila waumini wake lakini si kweli hao hao waumini wake si ndo wanao form hiyo serikali serikali bila waumini wake au chama bila waumini wake inakuwaje

    so kila mtu na dini yake bwana sisi tunawakataza na kuwapa ushauri wenzetu that is all hatutaki ku haribu party zenu

    wajui wenzao wanakwenda sunday school wao wameshoboka na vipati hata quran kusoma inawashindwa mabaro baro watu wazima na ndevu zao kama si hasara nini

    ReplyDelete
  16. mmepewa chance ya kupunguza makali ya maisha na stress zenu leo hii mnatudengulia mkifa kihoro na ma stress yenu msitutafute okay wanaotaka ku party njoeni jamani tuparty tu party maisha ndo haya na mafupi okay jumuiya oyeeee party party tunakuja kuparty party tunakuja kupunguza stress zetu

    ReplyDelete
  17. Hapo nyiyi waislam wa new york ndio hssara kwenu mnashindwa kushirikiana na kufungua madrassa. Miji mingi tu wameweza kama Toronto hata london. Wenzenu wakristo pia wnaendeleza dini yao.nyinyi kuiga tu party na sherehe zisizo na maana kwenu na watoto wenu Mkumbukeni Allah kwamba nyinyi ni wachinga na mtaulizwa juu ya mlichokichonga.

    ReplyDelete
  18. jamani kwani hizi party za jumuiya zinafanyika kila siku? sana sana nyingi ni 4 kwa mwaka. sasa hizo 4 ndo zitafanya mshindwe kuwapeleka watoto wenu madrasa jamani. you have 365 days in a year, siku 4 tu za party ndo zitake kuwa kisingizio!

    we human beings need social life as much as we need madrasa. we need to have balance in all areas of life. kama hamuelewi psychology basi ndo nawadokeza, the rest you can google.

    Happy party ya'll

    ReplyDelete
  19. jamani jamani mpoba mnakuja juu na kuwaonea watu waislamu watanzania wa new york au mnachuki nao binafsi si mseme tu huku maisha watu wanapambana nayo si mchezo si kubweteka ovyoo na tulikuwa hatuna viparty hivi sasa tumeanzima midomo juu kama chupa ya coca cola chunguzeni state zinginewe acheni unafiki wenu kwani lazima mtoto apelekwe madrasa si mzazi ukijua si unaweza pia kumfundisha nyumbani kwako.

    tuachiyeni tupumuwe kila mtu na kaburi lake wewe utakwenda peponi na sisi wacha tuende motoni okay usituone wajinga tunawafundisha watoto wetu majumbani hatutaki sifa na vijicho tupate vya watu kuwaona watoto wetu wako madrasa na wao watoto wao wako kwenye viuno party.

    ReplyDelete
  20. wenginewe bwana wanajidai tu kumbe wanafik wakubwa wanatamani waje kwenye party hii hawana uwezo wa kutoa hicho kiingilio ubahili umewashika ndo maana sasa wanasingizia mambo ya udini mara madrasa mara hivi na vile acheni unafiki wenu na wanajidai watu wa dini sana kumbe wanafik wazandik wakubwa kutwa kuwasema wenzao na kuwacheka na kujua umbeya wa vijumbani vyote na taabia chafu wanazo so wachamungu gani hawa.

    nendeni zenu na udini wenu kama hamtaki kuja kwenye party msije kaani makwenu au pigeni maboksi yenu na stress zenu mpaka mfeee na wala hatukutakini mje kwenye party yetu adheem

    WATOTO WAO WANAOJIDAI KWAMBA WAMEONGOKA KUMBE WANA MABOFRIEND NA MA GIRLFRIEND HUKO MASHULENI WAKIRUDI NYUMBANI HAO WATOTO WANAJIDAI WACHA MUNGU NA WAKATI MWINGINEWE WANAWATIA HAO MAGIRLFRIEND ZAO NA MABOYFRIEND ZAO NDANI YA NYUMBA WAKATIK WAZAZI HAWAPO WANAFIK WAKUBWA UNADHANI HATUYAJUI

    ReplyDelete
  21. Guys this is too much please! Cool down! Kila mtu afanye anavyotaka

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake