Askari Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam wakibeba maborota ya mitumba ya nguo za ndani kama sidiria na chupi leo katika soko la Karume katika operesheni ya kukataza kuuza nguo za ndani za mitumba ambapo operesheni hiyo ikiendeshwa na shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Marobota ya nguo za ndani yakipakizwa katika magari ya polisi leo wakati shirika la viwango Tanzania Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Nchini wakati walipoendesha operesheni Kataza kuuza nguo za ndani ambazo zishatumika(mitumba)
Askari Polisi wakiendelea na operesheni hiyo katika Soko la Karume huku wafanyabiashara wa Sokoni hapo wakishuhudia zoezi hilo
Magari ya polisi yakiwa Yamebeba Marobota ya Mitumba ya Nguo za Ndani mapema leo katika Soko la Karume katika Operesheni kataza kuuza nguo za ndani za mitumba
Msafara kuelekea katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi kwaajili ya kupeleka Mzigo uliokamatwa wa nguo za ndani zilizotumika almaarufu kama mitumba kwaajili ya kuteketezwa na moto wakati wa operesheni kataza kuuza mitumba ya nguo za ndani
kwa picha zaidi bogya soma zaid
kwa picha zaidi bogya soma zaid
Msafara wa polisi ukielekea Kituo Cha Msimbazi mapema leo mara baada ya Kukamata wafanyabiashara na bidhaa zao za nguo za ndani za mitumba
Msafara ukiingia Katika kituo cha Msimbazi
Mzigo Ukiwasilishwa katika kituo cha Polisi Cha Msimbazi Kwaajili ya kwenda kuteketezwa na Moto
Mmoja wa Wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akishusha sidiria za mitumba ambazo zimekamatwa leo katika operesheni kata kuuza nguo za ndani za mitumba
Mzigo Ukishushwa mara baada ya kufikishwa katika Kituo Cha Polisi Cha Msimbazi
Afisa Habari wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bi Roida akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukamata marobota ya nguo za ndani ambazo zimeshatumika wakati Nguo hizo zilishapigwa marufuku kuuzwa nchini.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
mnawaonea walala hoi mnawaonea watu maskini za mungu si kila mtu anauwezo wa kununua nguo za ndani za bei za madukani ni ghali mmno kwa mlala hoi mnawaonea maskini za mungu mungu anakuoneni nendeni mkawakamate wanaouza unga kuwaharibu watoto za watu na jamii ya kitanzania mbona mnawafumbia macho
ReplyDeleteHuu ni ushenzi .kuna mtu anakiwanda cha kutengeneza chupi na sidiria ndio kawapa pesa hawa tbs.kuna mambo muhimu yawakerao wananchi.chupi na sidiria,come on man
ReplyDeleteThis doesn't make any sense to poor Tanzanians, je huu ndo ukombozi kwa Mtanzania masikini? umeme juu, vyakula juu, kodi juu sasa watu watu wataacha kuvaa mitumba? Kama hiii serikali inajali kwanini isisaidie kupunguza ugumu wa garama za maisha, umeme, maji, elimu ili tuache mitumba. Hivi serikali inajali sana chupi tunazo vaa kuliko chakula na elimu inaleta maana gani. Tanzania amka...If government realy cares should distribute subsidize chupi all over the country. Nimaoni tu...
ReplyDeleteHawa polisi na TBS wanatakiwa wakakamate hizi nguo kwa wanaoagiza na sio hawa wauzaji wadogo wadogo maana huu ni uonevu haswaaa... Swali la kujiuliza(1) Ni kuwa hawa TBS na polisi wataenda kila kona ya jiji la Dar na vitongoji vyake au watakuwa wanazungukia hapo hapo Mchikichini. (2) Kama hizo ni nguo za ndani marufuku kwa kuwa wanazuia magonjwa, Je itakuwaje kuhusu mashati, fulana, bukta za mazoezi, soksi na hata suruali maana huko zinakotoka sio wote huwa wanavaa chupi hivyo basi kama ni ugonjwa basi utakuwa kwa nguo zote za mitumba na wazipige marufuku zote tu na kusiwepo na mitumba kabisa. (3) Kila mtu ana maamuzi yake ya nini afanye na kipi aache sasa kwa kuzuia hii biashara kwa wauzaji wakati hatuna hata kiwanda cha kutengeneza miswaki sidhani kama ni sahihi kwa kweli pia uwezo tunatofautiana sana tu hivyo kama mtu anaacha kitu kipya na kufuata alichokuwa na uwezo nacho nadhani ndio vizuri kwa sana kuliko kutojistiri kabisa... Hawa watu huwa wanakurupuka tu kama vile wapo usingizini na kuamua wanachotaka bila ya kufikiri mara mbili kuhusu hasara na faida, TUBADILIKEEEEEE...
ReplyDelete-PAKAJEUSI