Akizungumza na NIPASHE, Lyasuka ambaye ni mtaalam wa ukaguzi Uhamiaji, alisema haoni uhusiano baina ya uzalendo, usalama wa Taifa na uraia wa nchi mbili.
Alisema hata hapa nchini wapo raia (viongozi), wasio na uraia wa nchi mbili, lakini wameliingiza Taifa kwenye hasara kubwa.
“Ukizungumzia masuala ya kuhatarisha usalama; ubalozi wa Marekani ulilipuliwa mwaka 1998, je, aliyepiga mabomu alikuwa na uraia wa nchi mbili?” alihoji.
Alisema uhalifu ni kosa kama makosa mengine. “Tusije tukachanganya uraia wa nchi mbili na uhalifu, hivi ni vitu viwili tofauti,” alisema.
Alisema: “Kusema uraia wa nchi utahatarisha usalama wa nchi siyo kweli.
Uzalendo wa mtu upo moyoni mwa mtu bila kujali ana uraia wa nchi ngapi. Mtu anaweza akawa hapa Dar es Salaam au kijijini na akahatarisha usalama.”
Alisema kuhatarisha usalama ni kosa kisheria na kwamba mtu anayefanya hivyo anapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria.
Alisema Bunge Maalum la Katiba litafanya makosa makubwa kama litawanyima haki ya uraia Watanzania waishio nje ya nchi ambao wamepata uraia katika nchi wanazoishi.
Alisema kinachopaswa kutazamwa ni aina gani ya uraia akifafanua kuwa wanapaswa kupewa uraia pacha ni Watanzania wa asili siyo raia wa nje waliopewa uraia.
Lyasuka alisema Watanzania wengi walio nje ya nchi wapo kimkakati na kwamba fedha wanazopata huko watakuja kuwekeza au kujenga nyumbani, hivyo wasipopewa uraia wa Tanzania watashindwa kutimiza malengo yao.
Alisema hata sheria ya Uhamiaji ya mwaka 1995, kifungu cha 14, kinazuia mtu yeyote akiwamo Waziri wa Mambo ya Ndani kunyang'anya uraia kwa Mtanzania wa asili lakini katika hali ya kushangaza Bunge Maalum linataka kuwafutia haki hiyo.
Suala la uraia pacha liliwekwa kwenye rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, lakini Bunge Maalum la Katiba limefuta ibara hiyo baada ya serikali kueleza athari za kiuchumi na kiusalama kama jambo hilo litaruhusiwa kikatiba.
CHANZO: NIPASHE
6 comments:
Asante sana Mr. Lyasuka, Natumaini ujumbe utawafikia wahusika maana sababu zisizokuwa na msingi hupoteza muda na pesa.
Well said Sir, thank you for such great wisdom. You have said it all and blessed your heart because you put our nation interest first before personal interest.
Mhe. Zahoro Lyasuka, watu kama wewe ndiyo wanatakiwa waongoze nchi hii.
Huyu Lyasuka anatoa maoni tuu sio mtumishi wa serikali tena. Hakuna kitu hapa. Uraia pacha ni BOMU.
Ahsante ndugu Lyasuka, uzalendo ni mtu kujitoa na kusaidia Jamii yake kwa Hali na Mali vitu ambavyo wengi wetu tunafanya kuanzia kulipa karo za wanafunzi, matibabu ya wazazi, na kusaidia familia kwa ujumula. Huo ni uzalendo mkubwa sana.
Uarifu popote pale uwe ndani au nje ya nchi yoyote ile ni kosa hapo mkondo wa sheria utachukua nafasi yake. Kwa mfano ukifanya kosa Tz utashitakiwa Tz hata kama wewe una raia picha. Kuna Watu wanafanya makosa mijini,wanajificha vijijini. Wengine wanakimbilia mijini kutoka vijijini kwamba hakuna wa kuwajua kwenye wingi wa watu mijini. Kwa hiyo ni kazi ya vyombo vya sheria kufanya Kazi yake kuwatafuta watuumiwa popote pale ndani au nje ya nchi.
Kama wana takwimu watuambie kuna waTz wangapi wamefanya uarifu hapo nchini na kukimbilia nje na wameshidwa kuwakamata. TZ nchi yetu tuliyozaliwa ni sawa na baba na mama, na sijaona kuona wazazi wakamkataa mwanaye kisa mtoto anakaa nchi nyingine tofauti.
Wako Magai kutoka U.S
Wabunge wengi na uongozi wa serikali ya Kenya wanatambua faida za Wanadiapsora wao, lakini wabunge wengi na viongozi wachahe wa serikali ya Tanzania hawatambui kuelewa faida za watanzania waishio Ugaibuni. Wanatakiwa waelimishwe ili kuondoa ile tabaka ya vivu, uchoyo na kutoendelea kiuchumi. Hawa wabunge na viongozi wegine serikalini ndio waosema : Kaeni huko huko-mtakulaje huku na huko?
Sasa tunaishi dunia tofauti ambapo
uzalendo unapungua sana kwa sababu nchi nyingi zinajiunga pamoja kwa kiuchumi na kiutamaduni. Pili, kuhatarisha Usalama wa nchi ya Tanzania ni kichekesho kwa sababu Tanzania ni maskini mno na haina adui mpaka yesu arudi
Post a Comment