Advertisements

Monday, April 29, 2024

RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA JIJINI NAIROBI NCHINI KENYA






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi pamoja na Wageni mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.

WAZIRI BASHUNGWA ATOA MIEZI MIWILI KWA CRB NA NCC KUUNDA MABARAZA YA WAFANYAKAZI




Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumza katika uzinduzi wa Baraza la Wafanyazi la Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) na Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara hiyo na Taasisi zake, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour akitoa maelezo ya mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara hiyo na Taasisi zake, uliozinduliwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, jijini Dodoma.

Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Ujenzi wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyazi la Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) na Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara hiyo na Taasisi zake, jijini Dodoma.

RAIS DKT. SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA JIJINI NAIRONI NCHINI KENYA.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa Wimbo wa Taifa wa Kenya pamoja na ule wa Umoja wa Afrika (AU) ukiimbwa kabla ya kuanza Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mawaziri wa Kenya Musalia Mudavadi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.

DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZII WA SAUDI ARABIA NCHINI TANZANIA IKULU ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe.Yahya Bin Ahmad Okeish alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na ujumbe wake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe. Yahya Bin Ahmad Okeish, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Saudi Arabia Nchini Tanzania Mhe. Yahya Bin Ahmad Okeish, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameihakikishia Serikali ya Saudi Arabia ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo.

ZASP WAHIMIZWA KUTUMIA MTAALA MPYA WA ELIMU


Mkurugenzi Idara ya elimu ya Maandalizi na Msingi Fatma Mode Ramadhani akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Skuli binafsi wakati wa uchaguzi mkuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika Skuli Glorious Academy Mpendae.
Baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Skuli binafsi ZASP wakipiga kura kuchagua viongozi wa Jumuiya hiyo huko Skuli ya Glorious Academy Mpendae Wilaya ya Magharibi B.
PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR

Na Fauzia Mussa, Maelezo

Mkurugenzi Idara ya elimu ya maandalizi na msingi Fatma Mode Ramadhani amewataka wamiliki wa Skuli binafsi kutumia mtaala mpya uliotolewa na wizara ya elimu ili hakikisha watoto wote Zanzibar wanafundishwa kupitia mtaala mmoja.

Akizungumza na wanachama wa jumuiya ya skuli binafsi Zanzibar (ZASP) katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa jumuiya hiyo uliofanyika Skuli ya Glorious Mpendae Wilaya ya Magharibi B amesema kufanya hivyo kutawasaidia wanafunzi hao kujifunza mambo mbalimbali ya Nchi yao ambayo yamo katika mtaala huo.

SERIKALI YATOA BIL 1.5 UREJESHAJI MIUNDOMBINU YA BARABARA MWANZA

Serikali imetoa shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika maeneo mbalimbali Mkoani Mwanza.

Fedha hizo zimetolewa na serikali kwenda Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mwanza ili kuanza haraka kazi ya marekebisho miundombinu ya barabara na madaraja ambayo yameharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha

Meneja wa TANROADS Mkoa Wa Mwanza Mhandisi Paschal Ambrose ameyasema hayo wakati alipotembelea na kukagua uharibifu uliotokea kwenye barabara katika Wilaya za Nyamagana na Misungwi ambapo pia ametumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulioenezwa kwamba barabara katika eneo la Ng'ombe Wilayani Misungwi ni mbovu na haipitiki na amewataka wananachi kupuuza uvumi huo.

Amesisitiza kuwa Serikali imetoa fedha za dharura ambapo tayari wakandarasi wapo kazini wakiendelea na kazi.

Amesema miongoni mwa barabara zinazofanyiwa marekebisho ni barabara ya kutoka Mwanza kuelekea Musoma eneo la Nyamhongolo ambapo wanarekebisha mfereji ambao umeharibika kutokana na mvua hizo.

MAWAZIRI WA AFRIKA KUJADILI VIPAUMBELE VYA AFRIKA IDA 21


Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akipokelewa na Waziri wa Fedha wa Kenya Prof. Njuguna Ndung’u, alipowasili kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba, (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Kenya Dk. Chriss Kiptoo, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akisalimiana na Waziri wa Mipango Angola Victor Hugo Guiherme, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, jijini Nairobi, Kenya.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akiteta jambo na Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godogwana, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21) ngazi ya Mawaziri, unaofanyika tarehe 28 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.

RAIS SAMIA AWASILI NAIROBI KWA AJILI YA KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024. Rais Samia anatarajia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia unaotoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024. Rais Samia anatarajia kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia unaotoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha (kulia) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 28 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili Jijini Nairobi Kenya tarehe 28 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA

Sunday, April 28, 2024

RAIS DK.HUSSEIN MWINYI AZUNGUMZA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA JAMHURI YA SOMALIA IKULU NDOGO MIGOMBANI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe.Dkt.Hassan Sheikh Mohamud, na kutowa mkono wa pole kufuatiya kifo cha Baba yake Mzazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Mstaafu Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Migombani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 28-4-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe.Dkt. Hassan Sheikh Mohamud, baada ya kumaliza mazungumzo yao na kutowa mkono wa pole kufiatia kifi cha Baba yake mzazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Mstaafu Hayati Ali Hassan Mwinyi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Migombani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 28-4-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe.Dkt. Hassan Sheikh Mohamud, baada ya kumaliza mazungumzo yao na kutoewa mkono wa pole kufuatia kifo cha Baba yake mzazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Mstaafu Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Migombani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 28-4-2024

TUSIWATENGE WALA KUWANYANYAPAA WATOTO WENYE USONJI - MAJALIWA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuacha kuwanyanyapaa watoto na watu wanaoishi na Usonji, magonjwa ya mfumo wa fahamu pamoja na matatizo ya akili.
Pia amewataka wazazi na walezi wenye watoto wenye changamoto za ukuaji au uelewa watafute ushauri kwa wataalam wa afya ili watoto wao waweze kufaidika na huduma zilizopo katika umri mdogo.

"Wataalam wetu muendelee kuongeza juhudi katika kuelimisha jamii kuhusu magonjwa haya ili watu wengi zaidi waweze kunufaika na huduma."
Ametoa wito huo leo ( Jumapili 28, Aprili 2024) alipokuwa akizungumza baada ya kushiriki mbio fupi za hisani za Run 4 Autism Tanzania, zilizofanyika katika viwanja vya The Green Ground Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Kadhalika ameiagiza Wizara ya Afya kuongeza vituo vya huduma za uchunguzi hasa utambuzi wa mapema wa ugonjwa wa usonji na matatizo mengine ambayo yanaweza kubainika wakati watoto wanapoenda kwenye kliniki kila mwezi.

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS MOHAMUD WA SOMALIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud mara baada ya kuwasiliIkulu Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya Kiserikali tarehe 27 Aprili 2024.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud wakizungumza na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari mara baada ya Mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud na Ujumbe wake yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili, 2024.

SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SHULE BINAFSI- DKT. BITEKO


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi hususan shule binafsi ili kuboresha sekta ya elimu nchini.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Nchini (TAPIE), leo Aprili 27, 2024 jijini Dar es salaam Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan haiwezi kuacha Wadau wa Elimu wakilalamika, kwa kuwa uwepo wao unaisaidia Serikali.

“Nataka niwahakikishie kuwa Serikali imeendelea kukutana na TAPIE mara kwa mara, na hapa namuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama kuratibu mkutano wa pamoja kati ya TAPIE na Wizara za Ardhi, Fedha, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kujadiliana kwa pamoja na kupata suhulu ya changamoto zinazowakabili”, amesema Dkt. Biteko.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amewaasa TAPIE kuzingatia masharti yaliyoainishwa katika barua na vyeti vya usajili wa asasi zao, kwa kuwa kuna baadhi hukiuka masharti hivyo kusababisha migongano isiyo ya lazima na mamlaka zilizokasimiwa kusimamia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya uendeshaji wa asasi za elimu nchini.

RAIS DKT. MWINYI AKABIDHI KOMBE KWA SIMBA MSHINDI LIGI YA MUUNGANO


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhi Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Muungano Cup kwa Nahodha wa Timu ya Simba Mohammed Hussein, baada ya kuifunga Timu ya Azam katika mchezo wa Fainali uliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar,Timu ya Simba imeshinda mchezo huo kwa bao 1-0.






MAMBA WATISHIA USALAMA WA WANANCHI WA KATA YA RUVU.



NA WILLIUM PAUL, SAME.

MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka wananchi wa kata ya Ruvu kuwa makini na maji yanayotapakaa katika maeneo hayo kutoka mto Ruvu kutokana na maji hayo kuja na mamba ambao wanaweza kuleta madhara kwao.

Mkuu huyo wa wilaya pia amewaagiza Tarura kufika katika kata hiyo na kuona jinsi watakavyoweza kufungua njia ambapo kwa sasa maji yametapakaa kila mahali hali inayiwalazimu wananchi kutumia mitumbwi kutoka kwenda kutafuta mahitaji yao.

Kasilda amewataka kuacha kufanya shughuli za uvuvi wa samaki kiholela katika maeneo hayo kwani mamba hao wamekuwa wakiwakimbiza wananchi ambapo mpaka sasa Mwananchi mmoja ameshauwawa.

SERIKALI KUANZISHA TAASISI MPYA ITAKAYO TOA HUDUMA ZA UPASUAJI WA UBONGO NA MISHIPA



Rais wa Somalia Mheshimiwa Dkt. Hassan Sheikh Mohamud akitazama chumba cha upasuaji kilichowekwa mtambo wa matibabu ya moyo ‘Cathlab’ katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar Es Salaam leo Aprili 27, 2024. Rais H.S Mohamud amepokelewa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy mwalimu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.
Na WAF – Dar Es Salaam
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imedhamiria kuanzisha Taasisi mahususi ambayo itakuwa inashuhulikia masuala ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu ili iweze kuboresha zaidi huduma hizo za ubingwa kuitoa katika Taasisi ya Mifupa Ubongo (MOI) ambapo itabakia na masuala ya upasuaji wa mifupa pekee.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Aprili 27, 2024 baada ya uzinduzi wa chama cha madaktari bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu (Tanzania Neurosurgical Society) kikiongozwa na Rais wa chama hicho Dkt. Othmani Kiloloma Jijini Dar Es Salaam.