Akithibitisha taarifa hizo, kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema, maafa hayo yametokea katika kijiji cha Mwakata, kata ya Isaka, wilayani Kahama na kwamba watu wengine 60 wamejeruhiwa vibaya huku mifugo kadhaa, ikiwemo Ng'ombe, Mbuzi na kuku, navyo vimekumbwa na maafa. Huenda idadi ya waliokufa ikaongezeka, kwani zoezi la uokoaji linaendelea licha ya changamoto ya kutokuwa na vifaa vya kutosha vya uokozi.






hizi ni mvua za awali tu, je Serikali na miundo mbinu mko wapi bado mvua halisi za masika hazijaingia!! shughulikeni pungezeni siasa uchwra!!
ReplyDelete