ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 2, 2015

BIRTHDAY PARTY YA WEMA SEPETU NI KUFURU,

Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema Sepetu akiwa amesimama mbele ya meza iliyokuwa imesheheni keki alizokuwa amendaliwa katika sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa iliyofanyikia ndani ya Ukumbi wa Wema Sepetu Hall, uliyopo ndani ya jengo jipya la Millenium Tower.
Martin Kadinda (kulia), akimkabidhi ramani ya kiwanja Wema.
Wema akifurahia jambo wakati akionyesha zawadi ya gari lake jipya.
Meneja wa Wema (kushoto), Martin Kadinda, akimsaidia kukata moja ya keki zilizokuwa zimeandaliwa muda mfupi kabla ya kuanza kuwalisha ndungu jamaa na marafiki zake.
Nelly Kamwelu (kulia), kipiga picha ya pamoja na Wema.
Wema akimlisha keki mpenzi wake Luis Manana.
Wema akikisiana na mpenzi wake huyo baada ya kulishana keki.
Weama akiwa amekumbatiana na mpenzi wake.
Wema akiwa amekumbatiana na mama yake mzazi.
Steve Nyerere akiongea jambo mbele ya Wema wakati wa kulishana keki.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika pozi na Wema.
Wema akifutwa kitu kwenye kidevu chake na mpenzi wake.
Msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba (katikati), akitumbuiza kwenye Birthday hiyo.
Wema akiserebuka na dada zake kwenye hafla hiyo.
Badhi ya waalikwa wakishuhudia gari la Wema.
Muonekano wa ndani wa gari jipya la Wema.
Wema akiwa ndani ya gari yake mpya.MKURUGENZI wa Endless Fame Wema Sepetu, usiku wa kuamkia leo aliweza kufanya kufuru ya aina yake kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake iliyofanyikia ndani ya Ukumbi wa Wema Sepetu Hall, uliyopo ndani ya jengo jipya la Millenium Tower, Kijitonyama jijini Dar.
Katika Sherehe hiyo iliyohudhuliwa na ndugu jamaa na marafiki zake ilifana kwa kiasi kikumbwa, ambapo Wema alipewa zawadi mbalimbali huku akionyesha zawadi yake ya gari jipya aina ya Range Rover la mwaka huu.
Mbali na gari pia usiku huo meneja wake Martin Kadinda aliweza kuonyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo za Wema Sepetu ambazo zitakuwa zikiuzwa kwenye duka lake lililopo Mwenge TRA.

12 comments:

Anonymous said...

Sasa ubunge ulikuwa unautakia wa nini?

Anonymous said...

hivi huyu mdada uwa anafanya kazi gani mpaka awe na hela za ziada kununua gari kama hilo. ama ndiyo Tanzania yetu kila mtu anazungusha hela bila ya kujua shimbuko lake.Nakumbuka nilikuwa namwana kwenye kampeni za sisiemu baada ya uchaguzi hata rais kuapishwa tunaona mambo kama haya.

Anonymous said...

ccm oyeeeeeeeeee,i wish na mimi ningepata mchongo wa kampeni next election.

Anonymous said...

Mnona hayo ndio mambo ya ccm halafu mnasema hapa ni kazi tuu, hahaaaa ngoma ni ile ile ila wamembadilisha mpigaji

Anonymous said...

Wema kafanya kampeni gani za ccm??

Anonymous said...

Mwachen wema ccm ccm imefanya nini kwan hana pesa

Anonymous said...

Na mtatia akili wapambe ambao mnapiga schedule majuu au mliopo bongo mnaona onja joto alafu mnaimba mtaisoma namba wakati mwezenu kavuta mkwanja mrefu,nani mjanja Kati yake wewe na yeye?

Anonymous said...

Tuache mtima nyongo kabisaaaaa !!!!! CCM Wameshinda ni kweli hakuna ubishi. Je kila starehe ya Mtz ni sababu ya CCM ??? Huu ni ufinyu wa bongo. Tafuta kula ya kesho wewe na familia yako. Uchaguzi umepita mkuu na washindi wanawaza miaka 2020,2025 na zaidi itakuwa vipi. Bado la mkono 2015, Je bao la kifua 2020 utaliweza kulizuia. AFYA KWANA.

Anonymous said...

Yeye aliihama CCM na kumfuata Lowasa, nadhani Ukawa kishamkatia cheki na hicho ki-Range Rover. Ukitaka kulipwa kirahisi jiunge na Ukawa/Chadema. Toroka na Utakatiwa cheki.

Anonymous said...

Aka ni kamfano kadogo sana mtu anapewa mchongo sisiemu na ananunua gari lenye dhamani zaidi ya million 100 wakati Hana kazi wala biashara ya kueleweka. WaTZ tuwe na fikra Lowasa alisema nikipewa nchi elimu bure mpaka chuo kikuu watu wakauliza hela utatoa wapi?akajibu serikali ya sisiemu inanunulia mashangingi 200 million kila mtu, nikisimamisha kununua hayo magari ya kifahari ni hela tosha kwenye program hivyo pamoja na gesi asili. Nape wiki moja iliyopita alipata ajali na gari lake jipya lenye dhamani ya zaidi ya 200 million kazi yake ya sisiemu halipwi mshahara huyu na hana biashara kubwa ya kumpa kipato kama hicho.nadhani magufuli ana wakati mgumu sana kusafisha magugu hayo yote.

Anonymous said...

Haya ndio maisha watanzania wasio na elimu wanayataka, show off kwa hela za magumashi. Hawezi akakuelezea anapataje hela legally au bila kuuza uhuru. Sad to speak ndio watanzania walio wengi walio na akili za ubabaishaji. Hawaishi kwa purpose, tena ni wengi mnoo basi tu hawajapata michongo ya wanasiasa, na opportunity za ku-show off.

Anonymous said...

Nakubaliana na mdau 4:17am ,magufuli ana kazi kubwa sana,I feel sorry for him,huyu wema anapenda sana sifa na kutaka kumkomoa diamond tu hana lolote