Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamezungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya Jaji Mstaafu, Salome Kaganda ambaye ni Kamishna wa Maadili na Mtendaji Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwaandikia barua viongozi wa chama hicho akiwatuhumu “kukiuka masharti ya Hati ya Ahadi ya Uadilifu wa Viongozi wa Umma.”
Jaji Kaganda aliwaandikia barua viongozi hao tarehe 4 mwezi huu ambapo Chadema wameitaka sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kuacha vitisho kwa viongozi wa chama hicho.
Walioandikiwa barua hiyo ni Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema na Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.
Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, kwa mujibu wa barua ya Jaji Kaganda, katika tarehe, muda na siku ambayo haijulikani, viongozi hao wa Chadema walitoa matamshi ambayo yanachochea wananchi kutotii sheria, kufanya vurugu, kudharau misingi ya demokrasia iliyopo nchini na kutishia usalama wa nchi.
1 comment:
We need responsible political leaders from all parties, including Chadema. Regrettably, Lissu fails the test.
Post a Comment