ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 2, 2010

Mkenya sasa aanza kumkuna kocha Mourinho Inter


 Mcdonald Mariga PictureKIUNGO wa Kenya,ameanza kuonyesha makali katika Ligi Kuu ya Italia, Serie A.

Mariga, 22 alicheza kipindi cha kwanza katika kikosi cha Inter dhidi ya Udinese na kuishuhudia timu yake ikishinda na kuongoza kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya jirani zao, AC Milan.

Chipukizi huyo wa Kenya alisaidiwa na kukosekana kwa baadhi ya mastaa wa Inter .

Lakini, katika mchezo huo, Mariga alianza kuonyesha wasiwasi kabla ya kutulia.

Kocha wa Inter, Jose Mourinho alieleza kuridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo ambaye alisajiliwa mwezi Januari.

Katika mchezo huo, mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto'o, aliendelea kufanya vibaya tangu kuanza kwa mwaka huu.

Aliingia uwanjani dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Goran Pandev na hakucheza vizuri licha ya kutengeneza nafasi chache za kufunga.

Katika mchezo huo, Inter ilishinda 3-2 na kuwa na tofauti ya pointi nne dhidi ya AC Milan

No comments: