ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 17, 2010

Moto wateketeza makaburi ya wafalme Uganda

Falme za Baganda
Makaburi ya wafalme wa Buganda, maarufu kama makaburi ya Kasubi yameteketezwa na moto mkubwa mjini Kampala.
Makaburi hayo ambayo ni muhimu sana kwa watu wa ufalme huo pia yalikuwa yametambuliwa na shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, kama sehemu ya kihistoria.
Ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa kufuatia moto huo, msemaji wa polisi anasema kuwa afisa mmoja wa polisi amejeruhiwa baada ya kupigwa mawe na wananchi waliokuwa wamekasirishwa na tukio hilo.
Aidha magari matatu ya wazima moto nayo yaliharibiwa na umati uliotatiza juhudi za kuzima moto huo.
Mkuu wa polisi ameteua kamati maalum ya kuchunguza tukio hilo, ambayo itaongozwa na naibu mkuu wa CID Sakira Moses.
Wafalme wa nne wa Buganda wamezikwa kwenye makaburi hayo ya Kasubi yaliojengwa mwaka wa 1882 na Kabaka Mutesa wa kwanza na ndie aliyekuwa mfalme wa kwanza kuzikwa mahali hapo.
Moto huu umetokea wakati ambapo kuna mvutano kati ya serikali na ufalme wa Buganda.
Septemba mwaka jana watu kadhaa waliuawa, wengine kujeruhiwa na mali nyingi kuharibiwa kufuatia wa maandamano yakupinga hatua ya kumkataza Kabaka wa Buganda kuzuru eneo moja la Kayunga.

No comments: