ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 18, 2010

Simba wajilipia hoteli Zimbabwe


UONGOZI wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam umeamua kujigharamia chakula na malazi nchini Zimbabwe baada ya wenyeji wao kudai kuwa wanaukata wa fedha na wasingeweza kufanya hivyo kwa sasa.

Simba iliwasili Zimbabwe juzi tayari kwa mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Lengthens ya huko.

Mabingwa hao wa msimu huu walioshika nafasi ya pili msimu uliopita, wanaanza raundi ya kwanza wakati Lengthens waliitoa AS Adema ya Madagascar kwa jumla ya mabao 3-2

Baada ya kuwasili, msafara mzima wa Simba uligomewa kuingia hoteli waliyoandaliwa na wenyeji wao Lengthens ya huko kwa madai kuwa wenyeji wao hawajalipa fedha za kukaa hapo hatua iliyowafanya wachezaji wa Simba pamoja na viongozi wao kukaa nje hadi usiku.

Afisa Habari wa Simba, Cliford Ndimbo alisema kuwa kutokana na ukata uliowakuta wenyeji wao, ilibidi wajilipie hoteli iitwayo Creaster kwa dola 4,500 kwa makubaliano maalumu ya wenyeji kuwa watawalipa baadaye.

No comments: