ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 17, 2010

Sudan'yabana' ukweli kuhusu pato la mafuta


Shirika la kutetea haki, Global Witness linasema limefichua ushaidi unaonyehsa kuwa kumekuwepo na udanganyifu kuhusu mapato ya mauzo ya mafuta nchini Sudan.
Kulingana na shirika hilo, takwimu za kampuni ya China National Petroleum inayo chimba mafuta katika jimbo la Upper Nile zinaonyesha kipato chao kilikuwa asilimia 12 zaidi ya zile zilizochapishwa na serikali ya Sudan.
Uvumbuzi huu ni wa muhimu kwa kuwa Sudan kusini inategemea asilimia 50 ya kiptao hicho cha mafuta kulingana na mkataba wa amani wa mwaka 2005.
Lakini kwenye ripoti hiyo Global Witness, ipo makini isionekane kuwa inadai Khartoum inawafanyia hila wenzake kusini.
Hata hivyo hii ikiwa mara ya pili shirika hilo linatoa madai hayo bila shika hivyo ndivyo uongozi wa kusini utachukulia ripoti hiyo. Hata hivyo, serikali ya Sudan haijajibu madai hayo.
Tangu mkataba wa amani kati ya kusini na kaskazini usainiwe utwala wa Sudan kusini umepokea dola bilioni saba kutoka kwa mauzo ya mafuta.
Mwakani, raia wa kusini watapiga kura ya maoni kuhusu ikiwa watajitenga na kaskazini au la.
Na wakaazi wengi wa kusini hawaamini ikiwa utawala wa kaskazini utaunga mkono hatua yao ya kujitenga kutokana na utajiri wake wa mafuta.

No comments: